loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri aisifu Huawei kwa kukuza vipaji vya Tehama

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, kwa niaba ya Waziri Mkuu ameisifu kampuni ya Huawei Tanzania kwa kukuza vipaji vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika nyanja mbalimbali.

Imesema juhudi hizo zimesaidia na kuimarisha uwezo wa vijana kuweza kuajiriwa na kupambana na ushindani wa kazi za ndani ya nchi nan je ya nchi. Aliitoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya Tuzo ya Mashindano ya Huawei Tanzania Kuhusu Tehama 2019-2020.

Shindano hilo lina lengo la kutoa nafasi kwa vijana kuonesha vipaji vya Tehama na uwezo wao, kuwashindanisha, kuwawezesha kuwasiliana na kuwahamasisha kusoma masomo yanayohusu Tehama. Bashungwa alisema Tehama ni muhimu kwa maendeleo ya miundombinu ya Tanzania na lakini pia ni mwezeshaji mkubwa katika kufikia Dira ya Tanzania ya 2025.

Aliongeza kuwa katika mapinduzi ya viwanda, Tehama inabeba jukumu la msingi katika kujenga uchumi wa taifa, kutoa majibu kwa changamoto nyingi za kijamii, kuimarisha maendeleo jumuishi na endelevu kwa kukuza biashara, kutengeneza ajira na kuongeza tija na ufanisi.

Alisema pamoja na maendeleo ya haraka ya uchumi wa kidijiti duniani, ripoti ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia inabainisha kuwa mahitaji ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuhusu uhitaji wa ujuzi wa kidijiti ifikapo mwaka 2030 ni makubwa. Alisema nchini Tanzania, kuna uhaba wa wataalam wa Tehama katika sekta za umma na sekta binafsi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania, Frank Zhou alisema Huawei inaona kuwa imepata fursa muhimu kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na washirika wengine katika kuunganisha maeneo ya vijijini, kwa kujenga vituo vya gharama nafuu na vinavyotumia umeme wa jua.

“Huawei Tanzania inajivunia kuwa mstari wa mbele katika kujenga nguvu kazi ya kidijiti, kuwahudumia zaidi ya asilimia 35 ya Watanzania tangu tulipoanza shughuli zetu mwaka 2007, imetengeneza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 1,000 na kutoa mafunzo kwa wahandisi wa Tehama zaidi ya 2,000,”alisema Zhou.

Ili kukuza zaidi vipaji vya Tehama, Huawei Tanzania ina programu mbili zinazofanana. Programu ya kwanza ni haki ya kazi ambayo ilifanyika Julai 2019 na Programu ya pili ni mashindano ya Tehama, ambayo ni mchakato wa pili kwa mwaka wa utendaji wa Huawei Tanzania kushiriki hafla ya kidunia.

Zaidi ya wanafunzi 2,500 kutoka vyuo vikuu nchini, wanatarajia kushiriki shindano hilo litakalokuwa na mada mbalimbali, ikiwemo masuala ya mtandao na kompyuta. Kipindi cha usajili wa shindano hilo kilikuwa kiishe Novemba 22, wakati awali ilikuwa Novemba 27.

Hivi sasa, Huawei Tanzania iko tayari kutumia teknolojia zote ili kusaidia mageuzi ya kidijiti ya Tanzania. Wanafunzi waliosajiliwa, watapata vifaa vya kujifunzia na jalada la uthibitisho linalotolewa bure na Huawei.

WATAALAMU wa Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

JKCI yachunguza 150 shinikizo la damu Temeke

dakika 32 zilizopita Mwandishi Maalumu, Ukerewe

WATAALAMU wa Taasisi ya ...

Chagueni CCM, chama chenye mipango - Majaliwa

masaa 9 yaliyopita Mwandishi Wetu

MJUMBE ...

Mgombea CCM aomba kuchaguliwa tena

masaa 10 yaliyopita Alexander Sanga, Mwanza