loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchumi wa Zanzibar sasa wakua kwa 7.1 %

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema kuwa kasi ya ukuaji uchumi wa Zanzibar, imeongezeka na kufi kia wastani wa asilimia 7.1.

Alisema hayo wakati akifunga semina ya siku moja ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika ukumbi wa Taasisi ya Mafunzo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Mwanza. Rais Shein alisema kwamba mafanikio hayo yamepatikana kutokana na kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato hayo.

Alisema kuwa hali hiyo imeongeza mapato kutoka Sh bilioni 181.1 mwaka 2010 hadi kufikia Sh bilioni 748.9 mwaka 2018, ikiwa ni ongezeko la mara 4.1 sawa na asilimia 314.

Alizipongeza taasisi za TRA na ZRB zinazokusanya mapato. Rais Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba, imeongeza bajeti yake kwa mara 3.2 kutoka Sh bilioni 444.6 mwaka 2010/2011 hadi Sh trilioni 1.4194 mwaka 2019/2020. Aliongeza kuwa kutokana na ufanisi huo, hata bajeti za wizara mbalimbali nazo zimeongezeka ikiwemo Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

Alieleza kuwa huduma za jamii, nazo zimeimarika kutokana na mambo ya kisera yaliyopangwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 katika huduma za elimu na afya na kusababisha huduma hizo kutolewa bure.

Alisema Serikali ya Zanzibar imetoa umuhimu mkubwa katika kuhakikisha amani na utulivu, vinakuwepo nchini wakati wote na kwamba hali hiyo ndiyo iliyowezesha kupiga hatua kubwa za maendeleo katika nyanja ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Alieleza kuwa mafanikio hayo yote ya utekelezaji wa Ilani, yametokana na kuwepo kwa amani na utulivu, ambayo imetoa nafasi ya kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 na Muungano uliopo.

“Ibara ya 127 ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015-2020 inatuelekeza kuwa CCM itaendelea kuwa muumini wa kweli wa amani na utulivu na kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kuwa wamoja wenye mashirikiano na wanaopendana,” alisema DkShein.

Aleleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeanza kazi ya kuandaa Mwelekeo Mpya wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020-2050, baada ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa Dira 2020.

Alisisitiza kuwa Dira hiyo mpya ya Maendeleo ya Zanzibar, itakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2020-2030 na kuandaliwa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya 2020 kwa upande wa Zanzibar katika kuiletea maendeleo Zanzibar.

Alisema CCM imeimarika na inakubalika kwani imeweza kushinda katika chaguzi mbalimbali kwa sababu wananchi wanakikubali, hivyo aliwataka viongozi hao kuendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, huku akieleza kuwa kwa upande wa Zanzibar ushindi wa chama hicho katika uchaguzi ujao hauepukiki.

KUTOKANA na kazi iliyofanywa ...

foto
Mwandishi: Mwandihi Maalumu, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi