loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampeni dhidi ya kansa ya matiti, tezi dume kuzinduliwa leo

KAMPENI kubwa ya miezi miwili ya kupima saratani ya matiti na tezi dume inazinduliwa leo saa 4 asubuhi Tegeta kwa ndevu, GDB social Centre,darajani ilipo benki ya Mkombozi,Tegeta, Dar es salaam.

Kampeni hiyo inafanywa na Associazione Ruvuma Onlus taasisi iliyosajiliwa nchini Tanzania kama shirika lisilopata faida (NGO) ambalo hufanya kazi kwa karibu na serikali ya Tanzania, kwa kusaidiwa na Associazione Ruvuma Onlus ya Italia.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana,Rais wa Associazione Ruvuma Onlus ya Italia, Rodrigo Rodriquez alisema kwamba wameamua kufanya kampeni hiyo kwa kutambua umuhimu wa afya kwa wananchi na kwa taifa.

Alisema kampeni yao inasaidia juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ya kuwezesha afya kwa wananchi wake kwa kuwafanya wawe na hamasa ya kutambua afya zao na kudhibiti magonjwa ili kuwa na taifa lenye siha njema.

Alisema kampeni hiyo ya miezi miwili ya kwanza ya aina yake nchini itakuwa bure ikilenga wananchi wenye uwezo mdogo kipesa kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es salaam, idara ya Afya uchunguzi.

Alisema kansa inatibika ikiwahiwa na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza katika kampeni hiyo na wale watakaobainika kuwa na dalili za kansa au katika hatua za awali watafanyiwa mpango wa matibabu katika hospitali ya kansa Ocean Road na Muhimbili. Alisema pamoja na kufanya uchunguzi wa magonjwa hayo pia wataendelea kushirikisha wataalamu wa Italia katika masuala ya tiba.

“ Tunajitahidi ku-support (kusaidia) ufikiaji wa huduma za afya pamoja na kutoa mafunzo. Nipo Tanzania najiona nipo nyumbani. Nimekuwa nikifika hapa kwa takribani miaka 30 ni kama nipo nyumbani” alisema na kuongeza kuwa amekuwa akishirikiana na kanisa Katoliki katika kusaidia tiba.

Alisema kwamba ipo haja kwa mataifa ya Ulaya kulipa deni kwa waliyofanya Afrika zamani na deni hilo litalipwa kwa kuhakikisha wanapandisha uwezo wa mataifa ya Afrika kukabiliana na matatizo ya afya na elimu. Aidha alisema wakati alipofika nchini aliona shida iliyopo i na kuanzisha taasisi ya kusaidia maendeleo ya sekta ya afya nchini ya Associazione Ruvuma Onlus, Italia ambapo tayari imesaidia ujenzi wa hospitali na pia kutoa misaada mbalimbali ya vifaa tiba kupitia taasisi hiyo iliyopo hapa nchini Associazione Ruvuma Onlus (Tanzania).

Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Associazione Ruvuma Onlus (Tanzania), Happy Rwechungura katika mkutano huo alisema kwamba ipo haja kwa watanzania kujifunza kuchunguza afya zao mara kwa mara kwa kuwa tishio la kansa ni kubwa. Aidha alisema pamoja na uchunguzi huo kufanyika bure lengo ni kuona kwamba kansa inatibika na watu hawafiki kuomba tiba ya kansa ikiwa ipo katika hatua za mwisho.

Aidha alisema kwamba uchunguzi huo kwa mkoa wa Dar es salaam utafanyika katika vituo vya Tegeta mission Dispensary,Tegeta; Edward Muchaud Hospital iliyopo Sinza karibu na Kanisa la Kakobe;Consolata Mbagala Dispensary, Mbagala Mission na Cardinal Rugambwa hospital iliyopo Ukonga.

Anasema watakaofika katika vituo hivyo watafanyiwa uchunguzi kwa kutumia vifaa vya kisasa na kupata majibu na kwamba vituo hivyo vitakuwa wazi kuanzia asubuhi hadi jioni. Alisema kwa kampeni hiyo wanaunga mkono serikali hasa kwa kutambua kwamba serikali imeweka Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Saratani (The National Cancer Control Strategy (NCCS)-2013-2022) ambao ni msaada mkubwa kwa wadau kuchangia mkakati huo unaongoza maendeleo ya kitaifa ya kukabili saratani nchini.

KUTOKANA na kazi iliyofanywa ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi