loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kili Stars, Zanzibar Heroes kibaruani leo

TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na ile ya Zanzibar, Zanzibar Heroes zinatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye mechi mbili tofauti kusaka ushindi katika mchezo wa mwisho wa makundi ya michuano ya Kombe la Chalenji Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kilimanjaro Stars itachuana na Sudan huku Zanzibar Heroes ikitarajiwa kucheza na Kenya katika michezo itakayochezwa kwenye Uwanja wa KCCA, Kampala Uganda.

Ukiachilia mbali Kenya iliyokwisha kufuzu kwa pointi sita, Tanzania yenye pointi tatu, Zanzibar na Sudan zenye pointi moja, kila mmoja anaweza kuungana naye endapo zitashinda mechi zao za hatua ya makundi.

Kocha wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda, alisema wataingia kwa tahadhari na umakini mkubwa kwani wanajua hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu wanahitaji ushindi na Sudan itakuwa inahitaji kushinda ili ifikishe pointi nne.

“Vijana wako salama na wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) na tunajua utakuwa mgumu kwa sababu utatoa maamuzi ya nani atasonga mbele kikubwa ni kuwa makini tusirudie makosa,”alisema Mgunda.

Alisema amewapa wachezaji mbinu nzuri zitakazowapa matokeo na kurekebisha makosa yaliyoonekana katika michezo iliyopita.

“Umakini unahitajika kuhakikisha hawarudii makosa, waendelee kutuombea ili tupate matokeo mazuri,”alisema.

Naye kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Morocco alisema wapo tayari kwa mchezo na wanaamini watashinda na kufuzu nusu fainali. Katika michezo ya Kundi A iliyochezwa jana, Somalia iliifunga Burundi na kuondoka kwenye mashindano bila ushindi na Eritrea ikaifunga Djibouti kwa bao 1-0.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi