loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

U17 Tanzania Bara yaiadhibu Kenya

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 imeifunga Kenya kwa mabao 3-1 kwenye michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye Viwanja vya FUFA Technical Centre, Njeru, Jinja, Kampala.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa vuta nikuvute kila mmoja ikiwania kutoka kifua mbele kutokana na ukweli kuwa zote zina pointi nne. Katika mchezo huo Tanzania Bara ilianza kupata bao dakika ya 19 lililofungwa na Tabea Munga, bao lililodumu hadi mapumziko Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Tanzania Bara iliongeza bao la pili dakika ya 54 kwa penalti iliyotumbukizwa kimiani na Joyce Meshack.

Penalti hiyo ilitokana na mchezaji wa Kenya kuunawa mpira akiwa katika harakati za kuokoa Kenya walicharuka na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Fassila Adhiambo dakika ya 55 na Tanzania Bara ikafunga bao la tatu dakika ya 70 kupitia kwa Aisha Masaka. Katika mchezo mwingine Burundi iliifunga Djibouti mabao 8-0 na Uganda ikaifunga Eritrea kwa mabao 10-0.

Uganda wanaongoza wakiwa na pointi tisa ikifuatiwa na Tanzania Bara yenye pointi saba, Kenya inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne sawa na Burundi yenye pointi nne pia zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, Eriteria ina pointi moja na Djibouti haina pointi.

Mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mtindo wa ligi yatamalizika Desemba 17 yanatarajiwa kuendelea kesho ambapo Tanzania Bara itacheza na Uganda, Eritrea itaivaa Djibouti na Burundi itacheza na Kenya na baada ya michezo hii kila timu itakuwa imebakisha mchezo mmoja mmoja.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi