loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SGR kunufaisha wenye malori

CHAMA cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) kimesema kuwa ujio wa huduma ya treni ya kisasa ya mwendokasi itakayokuwa ikibeba mizigo na urejeshwaji wa huduma ya treni ya mizigo ya Dar es Salaam - Tanga hadi Moshi, itasaidia kuimarisha huduma za usafi rishaji wa mizigo za chama hicho.

Makamu Mwenyekiti wa Tatoa, Angelina Ngalula amesema hayo baada ya kuzindua ushirikiano na kampuni ya magari ya MFK ya hapa nchini na malori ya kubebea mizigo ya Hongyan ya nchini China.

Alisema wafanyabiashara chini ya Tatoa watashirikiana na serikali kupitia huduma za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli kutimiza azma ya kuiendeleza sekta ya usafirishaji nchini kufikia uchumi wa kati.

Ngalula alisema treni ya mizigo ikishasafirisha mizigo husika kutokea au kuelekea kwenye sehemu ya kuishushia, malori hayo ya Tatoa yataichukua kuipelekea sehemu ambayo huduma hiyo ya reli haifiki.

Alisema zipo fursa nyingi za usafirishaji na kusihi wafanyabiashara kuungana na kununua malori hayo.

Alisema Tatoa bado inaona imeelemewa kwa kuwa Tanzania imezungukwa na nchi nyingi zinatotumia huduma ya bandari za Tanzania na kuna idadi kubwa ya mizigo inayotakiwa kusafirishwa kwenda nchi hizo na amewashauri wafanyabiashara kuungana kuchukua mikopo taasisi za fedha kununua malori hayo.

Akizungumzia malori hayo alisema yanafungua milango zaidi katika nchi za Malawi na Zambia ambazo zilikuwa zikitumia malori kutokea kampuni za Afrika Kusini ambayo yameonekana kuwa na ubora zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MFK Automobile Tanzania, Ali Jawad Karmali amesema chini ya ushirikiano huo, Tanzania itakuwa kitovu cha vipuri vyote vya magari hayo. Alisema kuwa kampuni yake inayojihusisha na ukarabati wa magari, itaimarisha mtandao wa ukarabati wa magari kila kona ya nchi.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi