loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mzee Akilimali kuzikwa leo

ALIYEKUWA katibu wa baraza la Wazee la klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Ibrahim Akilimali amefariki dunia Alfajiri ya jana mjini Bagamoyo, Pwani. Akilimali alikutwa na umauti baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa ya Yanga kwa wanahabari jana ilisema Akilimali anatarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Tandale kwa Mtogole. Akilimali ambaye ni mzaliwa wa Kigoma amekuwa mpenzi wa Yanga tangu mwaka 1956.

Upenzi wake kwa Yanga ulizidi zaidi baada ya kuhamia Dar es Salaam mwaka 1966 kabla ya mwaka 1967 kuajiriwa kama mmoja wa wabeba mizigo wa bandarini, maarufu kama Kuli.

Alipata kadi yake ya kwanza ya uanachama wa Yanga mwaka 1972 na amewahi kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo kabla ya uteuzi wake katika Baraza la Wazee la klabu.

Akilimali atakumbukwa kwa misimamo yake zaidi ya kuitetea Yanga isimame kama ilivyo na si kuchukuliwa na watu kwa kofia za ukodishaji, au uwekezaji akipendekeza zaidi mfumo wa hisa.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi