loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barnaba- Walihisi nimekuwa shetani

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Elias Barnaba ametaja moja ya changamoto aliyokutana nayo wakati anaanza kuimba muziki kuwa ni wazazi wake kumkataza asijiingize kwenye sanaa hiyo kutokana na misingi ya dini ya familia yake.

Barnaba alisema kuwa wazazi wake walimfananisha na shetani kutokana na yeye kuamua kufanya muziki wakati wazazi wake wakiwa watumishi wa Kanisani.

Akizungumza juzi na EATV, msanii huyo zao la nyumba ya vipaji ( THT ) alisema wakati anaanza kuimba familia yake ilianza kumtenga kutokana na kuimba muziki maana haikutaka afanye hivyo.

“Mimi nilikuwa mtoto wa mtumishi wa Mungu, japo baadaye ikabidi nianze muziki na nikaingia THT,japo familia ikaanza kutaka kunitenga walihisi nimeshaharibika, nimeshakuwa shetani,” amesema Barnaba.

Amesema mara ya kwanza kufanya mahojiano na THT kwa ajili usaili, alishindwa kwenda kufanya mitihani shuleni na kwa bahati mbaya alikosa sehemu zote mbili, hivyo hata wazazi wake walishindwa kuelewa hatma yake.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi