loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kiir, Machar wakubaliana kuunda serikali ya umoja

Kiir, Machar wakubaliana kuunda serikali ya umoja

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir na aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar, wameingia makubaliano ya kutengeneza Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayojumuisha pande zote mbili, ingawa wameshindwa kutatua tofauti zao zote kabla ya tarehe ya mwisho waliyokubaliana Viongozi hao wawili mwaka jana walisaini mkataba wa amani wa kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka mitano nchini humo, ikiwa ni msukumo kutoka jumuiya ya kimataifa.

Kiir na Machar waliamua kurudisha nyuma utekelezaji wa mkataba huo kwa siku 100 kabla ya tarehe ya makubaliano na kuamua kumaliza vurugu mapema zaidi kwa makubaliano ya kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa.

“Tumesema kuwa, baada ya siku 100 ni lazima tutengeneze serikali ya umoja wa kitaifa, lakini kama maandalizi yatakuwa hayajakamilika basi tutatengeneza serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa kuanza utekelezaji wa mambo muhimu,” alisema Rais Kiir kwa waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya siku tatu baina yake na Machar mjini Juba.

Pande zote mbili zimekuwa zikitupiana lawama kwa kushindwa kukamilisha matakwa ya mkataba kutokana na kutokubaliana juu ya idadi ya majimbo ambayo nchi inapaswa kuwa nayo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011. Machar alisema wameshajadili kuhusu suala la majimbo na mipak, lakini hawajafika mwafaka.

“Tumeshazungumza kuhusu masuala ya majimbo na mipaka, lakini bado hatujaafikiana masuala kadhaa,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0e31d4add389bd24a3b78d1e65cd1cda.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: JUBA, Sudan Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi