loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TRA Shinyanga yapangiwa kukusanya bilioni 24.9

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga imepangiwa kukusanya Sh.bilion 24.9. Kufikia malengo hayo, imetaka wateja na wafanyabiashara kutoa na kupokea risiti wakinunua bidhaa.

Ofisa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka mamlaka hiyo, Antony Fabian alisema hayo kwa waandishi wa habari katika semina ya uelewa kuhusu umuhimu wa mashine za kodi za kielektroniki (EFD), ongezeko la thamani (VAT) pamoja na elimu ya mlipakodi kwa utaratibu uliowekwa na serikali.

Alisema TRA mkoa wa Shinyanga katika bajeti ya sserikali ya mwaka 2019/2020 ya Sh trilioni 33.11, mkoa umepangiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 24.9 huku lengo nchi nzima likiwa Sh triloni 19.1.

“TRA mkoa wa Shinyanga kila mwezi hukusanya Sh bilioni mbili. Nawashauri wafanyabiahara watumie mashine za EFD bila kukwepa na wateja wadai risiti. Watu wengi wanadhani kodi inakatwa kupitia mashine hiyo. Siyo kweli, inatunza kumbukumbu ya kutambua kipato kilichoingia kwa mwezi,” alisema.

Alisema wapo baadhi ya wafanyabiahara wanakwepa kutumia mashine za EFD kwa lengo la kutoonesha uhalisia wa biashara zao ili mauzo yaonekane kidogo na hiyo ndio njia ya kupoteza mapato ya serikali .

Alisema baadhi ya wafanyabiashara wananunua mashine za EFD na kutozitumia huku wakitoa taarifa za uongo. Alisema watu wa namna hiyo hupewa adhabu ya faini Sh 5,000,000 au kifungo miaka mitatu.

Pia alisema wapo wateja wamekuwa hawadai risiti jambo ambalo ni kosa kisheria hivyo atakayebainika atastahili kutozwa Sh 30,000 hadi Sh milioni 1.5 kwa kutegemea na makosa yaliyoambatana nayo.

Fabian alisema mashine za EFD zikipata hitilafu ni wajibu wa mfanyabiahara mwenyewe kutoa taarifa kila wakati kwa wasambazaji wa mashine hizo na watoa huduma TRA zirekebishwe biashara iendelee.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi