loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijana wa kujitolea JKT waitwa kupewa ajira

SERIKALI imetangaza ajira kwa vijana wote wenye shahada ya kwanza, waliohudhuria na kuhitimu mafunzo ya ‘t’ na kujitolea kufanya kazi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Sasa vijana hao wametakiwa kupeleka taarifa binafsi Ofisi ya Utumishi ndani ya siku 10 kuanzia jana. Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dk John Magufuli ya kutaka vijana wote wenye shahada ya kwanza, waliohudhuria na kuhitimu Operesheni Magufuli ambao wamejitolea kufanya kazi JKT, wapewe ajira serikalini.

Akizungumza jana jijini hapa, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema watakaonufaika na fursa hiyo ni wale waliojitolea na kuendelea kufanya kazi kwenye makambi ya JKT kwa kipindi cha miaka miwili.

“Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameamua kujitolea na kuendelea kufanya kazi kwenye makambi mbalimbali ya JKT kwa moyo na kujitolea, kwa kutambua mchango wao wa kujitolea Rais Magufuli alitoa maelekezo ya vijana hao wenye shahada ya kwanza waajiriwe na sisi tumeanza kulitekeleza hilo,” alisema Dk Ndumbaro.

Alisema vijana hao wanatakiwa kuwasilisha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora taarifa binafsi (CV), vyeti vya elimu, taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya JKT vilivyothibitishwa na JKT.

“Vijana hao wanatakiwa kuwasilisha taarifa binafsi, vyeti vya elimu na taaluma na vya kuhitimi JKT ili serikali iweze kuona namna ya kuwatumia vijana hao kwa kuwapata ajira katika maeneo mbalimbali ya serikalini,” alisema.

Aliongeza kuwa taarifa wanatakiwa kutuma kwa baruapepe ps@ utumishi.go.tz kuanzia jana hadi Januari 1, 2020. Alipoulizwa ni taaluma zipi ambazo vijana hao wataajiriwa, Dk Ndumbaro alisema tathimini ya awali ilionesha kuna takribani vijana 800 ambao wana sifa hizo na kuwa wote wenye sifa wataajiriwa.

“Kwa mwaka 2019/2020, serikali ilipanga kuajiri watumishi zaidi ya 40,000 ambazo tunatarajia kuanza kuzitoa mwezi Februari mwakani, katika nafasi hizo tumetoa fursa ya kuajiri vijana wote wenye shahada na waliojitolea JKT na wote tutawachukua maana walikuwa hawazidi 800 hivi,” alieleza.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi