loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Msiotoa gawio ondokeni saa 6 usiku Januari 23’

WENYEVITI bodi na wakuu wa taasisi na mashirika 50, ambao hazijatoa gawio katika Mfuko Mkuu wa Serikali, wanatakiwa kuwa wamejiondoa wenyewe kwenye nafasi zao ifi kapo saa sita kamili usiku, Januari 23, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisisitiza mashirika na taasisi hizo, zinatakiwa kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli la siku 60 kuhakikiza wanatoa gawio.

“Hadi sasa bado taasisi na mashirika 50 ambazo hazichangia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, narudia kusisitiza kuwa wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi na mashirika husuka watekeleza maelekezo ya Rais, la sivyo waondoke kwenye nafasi zao ifikapo saa sita kamili usiku, Januari 23, 2020,” alisema Dk Mpango.

Dk Mpango alisema hadi kufikia Desemba 30, 2019, jumla ya Sh trilioni 1.072 zimekusanywa ikilinganishwa na Sh bilioni 673.502 zilizokusanywa kutoka taasisi na mashirika ya umma 46 katika kipindi cha mwaka 2017/18.

Alisema makusanyo ya mapato kutoka katika taasisi na mashirika ya umma 79 kwa mwaka 2018/19, yalikuwa Sh trilioni 1.053. Alisema makusanyo hayo kutoka taasisi na mashirika 79 ni kati ya mashirika na taasisi 266, ambazo hadi Novemba 24, 2019 ziikuwa zimetoa gawio mbele ya Rais Dk John Magufuli.

Alisema kati ya mashirika na taasisi 266 za serikali, 187 zilikuwa hazijawasilisha gawio na michango katika Mfuko Mkuu wa Serikali katika kipindi chote hadi Novemba 25, 2019.

Dk Mpango alisema kuanzia Novemba 25, 2019 hadi Desemba 30, 2019, mashirika na taasisi 137 yaliwasilisha gawio katika mfuko mkuu wa serikali katika kutekeleza agizo la Rais, ambazo jumla zilichangia Sh bilioni 19.6. Alisema hadi kufikia Desemba 30, 2019, jumla ya Sh trilioni 1.072 zimepatikana licha ya taasisi na mashirika 50 kutotoa gawio katika mfuko mkuu wa serikali hadi sasa.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi