loader
Picha

Asifu serikali ya JPM kuvipatia umeme vijiji 277 mkoa Pwani

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (pichani) amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuutengea mkoa huo Sh bilioni 50 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya umeme vijijini.

Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Pwani, alilipongeza Shirika la Umeme (TANESCO) kwa kufanya miradi kwa fedha zake za mapato ya ndani na kuwaunganishia umeme wananchi wa vijiji wa vijiji 277 hadi sasa. Alisema hayo katika Kitongoji cha Mtakuja Kijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo wakati akiwasha umeme kwenye kitongoji hicho.

Mgalu alisema mkoa huo umetengewa fedha hizo kwa ajili ya miradi ya umeme kwenye vijiji ambavyo havina umeme kwenye mkoa huo, ili ifikapo 2021 vijiji vyote viwe na umeme. Kwamba huo ni mpango wa nchi nzima.

“Fedha hizo zimetengwa na serikali ambapo kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa umeme, hivyo tunampongeza Rais Magufuli kwa kututengea kiasi hicho kikubwa,” alisema Mgalu.

Akizungumzia shirika hilo, alisema kuwa hadi sasa limewaunganishia umeme wananchi hao kwa bei ya Sh 27,000 tu, kama alivyokuwa anafanya Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Anasema huo ni mwanzo mzuri kwa shirika hilo.

Alibainisha kuwa hivi sasa Tanesco imebadilika, kwani inaweza kutekeleza miradi yake kwa fedha zake, mbali ya fedha zinazotolewa na wafadhili mbalimbali. Kwamba kipindi cha nyuma, wananchi walikuwa wakiunganishiwa kwa fedha nyingi. “Nawapongeza na huu ni mwanzo mzuri, mmeonesha kuwa mnaweza miradi kama hii, kipindi cha nyuma ilikuwa inatekelezwa kwa gharama kubwa, lakini mmeonyesha kuwa mnaweza,” alisema Mgalu.

Kwamba hivi sasa shirika linawafuata wateja majumbani na si kuwasubiri ofisini, hivyo kuongeza idadi ya wateja na kukabili changamoto za ukosefu wa umeme hasa vijijini. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Fukayosi, alisema kuwa kuna baadhi ya vijiji, bado havijafikiwa na umeme.

Ally alisema kuwa mbali ya vijiji hivyo kutokuwa na umeme, pia shule ya msingi ya kitongoji hicho haina umeme. Aliishukuru Tanesco kwa kuunganisha wale wote ambao wamekamilisha taratibu na malipo, kwani wataunganishiwa umeme ndani ya siku tatu.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Bagamoyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi