loader
Dstv Habarileo  Mobile
Liverpool ndio timu pekee ambayo haijafungwa Ulaya

Liverpool ndio timu pekee ambayo haijafungwa Ulaya

LIVERPOOL imeweka rekodi ya kuanza msimu bila kufungwa hadi sasa kwenye ligi kuu tano za Ulaya baada ya juzi kuifunga Tottenham kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Roberto Firmino ambaye alifunga bao pekee aliwakikishia mabingwa hao wa Ulaya kuwa juu kileleni kwa tofauti ya pointi 16 wakifuatiwa na Leicester City. Liverpool katika michezo 21 iliyocheza imewafanya kuwa kileleni wakiwania taji la Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 30, ambapo Klopp ameona dalili za kuwa bingwa.

“Tunajua kuhusu hilo na ni muhimu lakini siwezi kukisia,” alisema Klopp.

“Mtu akikupa kombe, anafanya lakini unahitaji kulipigania. Ni mwanzo tu. Tunahitaji kuendelea kwa sababu wapinzani wetu wana nguvu.

“Pep Guardiola kocha wa Manchester City hajakata tamaa, Nitafanya vivyo hivyo, kufikia hapa tupo vizuri sana,” alisema Klopp.

Rekodi inayoendelea kutunzwa London na mshambuliaji raia wa Mbrazil Firmino, aliyewageuza vijana wa Spurs Japhet Tanganga na kumfunga Paul Gazaniga kwa mguu wa kushoto iliwafanya wageni kuonekana wanaostahili kuwa kileleni.

Liverpool walishukuru umalizia mbaya kwa upande wa Jose Mourinho ambao walimkosa Harry Kane ambaye ana jeraha ili kuandika ushindi mwingine kwenye safari yao ambayo ilionekana kuwa ngumu kutwaa taji la kwanza katika miongo mitatu.

Son Heung-Min na mbadala wake Giovani lo Celso aliyeingia kuchukua nafasi yake walikosa nafasi nzuri za kufunga katika nusu ya pili, Spurs kwa kiwango chake kilichoboreka katika mchezo huo.

Lakini Liverpool wamezidi kuiacha Leicester City katika msimamo baada ya kupoteza kwa Southampton na kuongeza utofauti mkubwa wa pointi katika kuwania ubingwa msimu huu wa ligi kuu. Liverpool inaweza kuwa haikufanikiwa kwani kulikuwa na makosa katika kipindi cha pili lakini ni timu iliyoonekana hazuiliki kulikaria taji la ligi kuu.

Huo ni ushindi wao wa 12 mfululizo wa ligi na wamepoteza alama mbili tu kutoka kwa michezo 21 waliyocheza. Kocha wa Tottenham Hotspurs, Jose Mourinho aliiambia BBC kuwa : “Huu ni mpira wa miguu. Wakati mwingine unapata zaidi ya unavyostahili na wakati mwingine unapata kidogo na katika mchezo huu hatukupata chochote wakati tulistahili. Hii ni timu bora ulimwenguni dhidi ya timu ambayo ipo katika wakati mgumu wa majeraha, katika msimu. Wachezaji walicheza vizuri na walijaribu kubadilika na kutengeneza nafasi,” “Sikuiangalia.

Ninachotazama ni 200% ambayo imetupa kuanza lengo lilikuwa kutupwa kwa bao letu. Nimechanganyikiwa kwa sababu hiyo na VAR ,” Alipoulizwa juu ya kumalizika katika nafasi nne za juu alisema: “Inawezekana kuzungumza juu ya nafasi nne za juu wakati unapoanza msimu kwa alama sifuri. Lakini ni ngumu kuizungumzia wakati unapoanza kwa dakika 12. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, aliambia BBC: “Ilikuwa ngumu sana kwa sababu hatukufunga bao mapema.

Tulipaswa kuwa tumefunga mabao 2-0 wakati tulipofunga. Ikiwa una mpinzani wa ubora kama Tottenham na hautafunga mchezo wao, Allison hufanya mambo yaonekane rahisi,” Kwenye kujihami alisema: “Tulimhitaji Allison, tulikuwa na dipu chache kwa kujihami. Michezo mingine hajapata kushinda mapema, ni nzuri lakini hakuna nafasi nyingine ya kushinda michezo kuliko kutetea vizuri,” alisema Klopp.

Tottenham Hotspur wamefunga mabao 20 katika mechi 13 katika mashindano yote wakiwa na Jose Mourinho wakati akiwa Chelsea alitumia michezo 44 kupata mabao 20 katika msimu wa 2004-05. Tottenham itaikaribisha Middlesbrough katika mchezo wa FA Cup raundi ya utakaochezwa kesho 14 na Jumamosi watasafiri kucheza na Watford in t katika mchezo wa ligi kuu wakati Liverpool wataikaribisha Manchester United kucheza mchezo wa ligi kuu Jumapili ijayo, Anfield.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/27140b16444bfd928aeb7a02412a8dd8.jpg

OLE Gunnar Solskjaer amesema, kuwasili kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi