loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serena ashinda taji la kwanza tangu aitwe mama

Serena ashinda taji la kwanza tangu aitwe mama

MCHEZAJI wa Tenisi, Serena Williams ameshinda taji lake la kwanza baada ya miaka mitatu tangu kuwa mama kwa kumfunga Jessica Pegula kwenye mashindano ya Auckland Classic.

Bingwa wa zamani mara 23 wa Grand Slam alipiga Mmamerika mwenzake kwa seti 6-3 6-4. katika mchezo ambao ulitumia saa moja na dakika 35. Serena mwenye umri wa miaka 38, mara ya mwisho alishinda tuzo ya Australian Open mwaka 2017 katika mashindani ya 73 ya WTA akiwa mshindi wa jumla.

Serena katika muongo wake wa nne kwenye WTA, alipoteza fainali za Wimbledon na US Open mwaka 2018 na 2019 na katika fainali ya Kombe la Roger mwaka 2019 alijiondoa.

Alisema baada ya ushindi wake atatoa pesa zake za zawadi za Auckland na mavazi atakayoshinda kusaidia Australia katika maafa ya moto. “Nimekuwa nikicheza kwa muda mrefu sana na kupitia hili nimefurahi kufanya kitu ninachokipenda,” alisema Serena.

“Ninajiona nina bahati na nimebarikiwa kuwa hapa na kuwa na afya njema na kucheza.”

Ufunguzi wa Australia Open utafanyika Januari 20, na Serena akitoa rekodi sawa na Margaret ya mataji 24 ya Grand Slam. Serena alishinda taji lake la kwanza la WTA Februari 1999, wakati alipopiga Amelie Mauresmo wa Ufaransa huko Open Gaz de France.

Alianza pole pole Auckland, na Pegula akichukua 3-1 katika seti ya kwanza na baadaye kushinda michezo mitano iliyofuata na kufunga seti za ufunguzi. Serena alianza kumfunga Pegula mapema seti ya pili na akabadilika hatua yake ya nne ya mechi ili kuhakikisha anapata ushindi.

Alisherehekea kwenye uwanjani na binti yake, Olympia, ambape alikuwa na ujauzito wa wiki nane wakati akishinda taji lake la mwisho la Grand Slam huko Melbourne. Jumapili ijayo atacheza kwenye hatua nyingine na Caroline Wozniacki wakicheza na Asia Muhammad na Taylor Townsend kwenye fainali ya wachezaji wawili.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e90678178c78148799d70432f7500ecf.png

Mambo yamaenza kuvurugika kunako klabu ya PSG, baada ...

foto
Mwandishi: AUCKLAND, Australia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi