loader
Dstv Habarileo  Mobile
Uuzaji wa silaha waiingizia Urusi mabilioni

Uuzaji wa silaha waiingizia Urusi mabilioni

NAIBU Waziri Mkuu nchini Urusi, Yuri Borisov amebainisha kuwa nchi hiyo imekuwa ikiingiza takribani Dola za Marekani bilioni 14 hadi 15 kwa mwaka, kutokana na kuuza silaha nje ya nchi.

Sehemu ya uzalishaji wa raia katika muundo wa pato la tasnia ya ulinzi ya Urusi iliongezeka kutoka asilimia 20.9 mwaka 2018 hadi asilimia 24.1 mwaka jana. Sehemu ya uzalishaji wa raia ilifikia asilimia 34.1 mwaka jana katika ujenzi wa ndege, asilimia 14.6 katika tasnia ya umeme na asilimia 19.1 katika ujenzi wa meli alisema Borisov akinukuu takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara.

Lengo la Rais wa Urusi ni kuhakikisha uzalishaji wa raia katika muundo wa tasnia ya ulinzi unaongezeka na kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 na asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a81f16cfa3489779525132dcb6a23a63.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi