loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ndege yawamwagia wanafunzi mafuta ikitua kwa dharura

Ndege yawamwagia wanafunzi mafuta ikitua kwa dharura

NDEGE ya abiria imemwagia mafuta shule kadhaa nchini Marekani wakati ikiajiandaa kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angels. Takribani watu 60, wengi wao wakiwa wanafunzi wanapatiwa matibabu ya ngozi na kupumua baada ya kuathirika vibaya na mafuta hayo.

Mafuta ya ndege mara kadhaa humwagwa ili kuiwezesha ndege kutua kwa dharura lakini mara nyingi marubani hutafuta maeneo yaliyojitenga kwa mujibu wa Sheria za Anga.

Hata hivyo, ndege ya kampuni ya Delta ilijikuta ikimwaga mafuta hayo maeneo ya makazi baada ya kuahirisha safari yake na kurejea uwanja wa ndege baada ya injini yake kupata hitilafu. Watoto wote pamoja na watu wazima walioathiriwa na mafuta hayo yaliyoathiri takribani shule sita, wamepatiwa matibabu na kwamba ni wachache ndio wamepata madhara makubwa.

Shule ya Park Elementary iliyopo mji wa Cudahy, ambayo iko kilometa 26 kutoka uwanja wa ndege wa Los Angele ndio iliyoathirika zaidi kwani wakati ndege hiyo inamwaga mafuta wanafunzi wa madarasa mawili walikuwa nje.

Meya wa Cudahy Elizabeth Alcantar, alisema amesikishwa na tukio hilo kwani mafuta mengine yameathiri shule ya awali ambayo ina watoto wadogo sana. Kampuni ya ndege ya Delta imethibitisha kupitia taarifa yake kuwa ndege hiyo ya abiria ililazimika kumwaga mafuta hayo ili kupunguza uzito wakati ikitua kwa dharura.

Msemaji wa Shirika la Anga la Los Angeles Allen Kenitzer, alibainisha kuwa tukio hilo linafanyiwa uchunguzi kwa kuwa sheria za anga ziko wazi inapolazimika kumwaga mafuta inatakiwa ifanye nini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/02b358894637873832fd45187cb07fa9.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: LOS ANGELES, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi