loader
Picha

Mahabusu wadai kunyimwa chakula, mmoja azimia kortini

RAIA wa Burundi, Habonimana Nyandwi ambaye anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya tembo, Wayne Lotter amezimia mahakamani ikidaiwa hawajapata chakula kwa siku tano hali inayochangia kudhoofu.

Nyandwi na washitakiwa wenzake walipanda kizimbani jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Godfrey Isaya ambapo kesi yao ilikuja kwa ajili ya kutajwa. Kabla ya kupanda kizimbani mshitakiwa Nyandwi alishindwa kusimama na kudondoka chini huku akionekana kugeuza macho, ndipo askari polisi waliokuwa karibu walipomsogelea na kumvua viatu pamoja na mkanda.

Kutokana na hali hiyo, mshitakiwa Zebedayo alinyoosha mkono na kuangua kilio kwa nguvu akidai raia wa kigeni waliopo kwenye kesi hiyo hawana ndugu wala mtu yeyote anayeweza kuwapatia chakula.

Alidai wamedhoofika kwa sababu gereza la Keko limewakatia huduma ya chakula raia wa kigeni hivyo hawajala kwa siku tano. Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Ester Martin alidai mahabusu wote wanapatiwa huduma za chakula pamoja na malazi magerezani hivyo, suala hilo ni vema, wakaulizwa magareza na kwamba upelelezi uko hatua za mwisho na jalada lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitakia nchini (DPP).

Hata hivyo, askari magereza alipoulizwa kuhusu tuhuma za watuhumiwa hao kutopewa chakula, aliieleza mahakama kuwa hana taarifa zozote kuhusu jambo hilo kwani anachofahamu yeye mahabusu wote wanapata chakula. Mshitakiwa Ayubu Selemani alidai, katika mahabusu ya Keko kuna raia wa kigeni wengi na wote wanapata chakula kwa wakati isipokuwa wawili hao waliopo kwenye kesi hiyo ambao wamekatiwa huduma siku tano.

Alidai waliitwa na Ofisa Usalama wa Keko na kuambiwa kuwa hawatapewa chakula na kwamba walipojitahidi kwenda kumuona bwana jela kupeleka malalamiko yao, askari wa kawaida wanawazuia. Alidai juzi ndio walifanikiwa kumuona bwana jela ambaye naye aliwaambiwa washitakiwa hao hawawezi kupewa chakula.

Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu ili kupata taarifa juu ya malalamiko ya washitakiwa hao. Mbali na washitakiwa hao katika kesi namba 9/2017 wengine ni Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi, Robert Mwaipyana, wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A, Innocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Wengine ni Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37) mkazi wa Mbagala B na Mohammed Maganga (61) mchimba makaburi, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Selemani, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Katika kesi ya msingi washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter. Washitakiwa hao wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wanadaiwa kumuua Lotter.

MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amewashauri viongozi wanawake, ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi