loader
Picha

Magufuli kuongea na madaktari Machi 4

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni katika siku ya madaktari nchini ambayo itafanyika Machi 4 kwenye ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)

Akizungumza na Habari Leo, Rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Elisha Osati alisema kuelekea siku hiyo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya kitabibu ikiwemo kutoa huduma za vipimo na matibabu ya kibingwa bure kwa wananchi nchi nzima.

“Nchi yetu kwa sasa imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya, kuna matibabu mengi ya kibingwa ambayo yanafanywa hapa nchini siku za nyuma yalikuwa hayapatikani, onyesho hili lengo ni kuitangaza nchi kimataifa ili nchi za Afrika zinazotuzunguka ziweze kutambua na kuleta wagonjwa wao Muhimbili badala ya kukimbilia India na nyingine,” alibainisha.

Baadhi ya huduma za Kibingwa zinazotolewa nchini kwa sasa kupitia hospitali ya Taifa ya Muhimbili Upanga, Muhimbili Mloganzila, Benjamini Mkapa Dodoma na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (J KCI) ni upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo kwa mtambo wa Cathlab, Kuzibua mishipa ya moyo kwa kutumia paja au mkono, upandikizaji wa figo, vipandikizi vya kusikia, upandikizaji wa uruto kwa wagonjwa wa saratani na selimundu, upandikizaji wa nyonga na upasuaji wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu.

Alisema siku hiyo ya madaktari itaenda sambamba na kambi mbalimbali za kitabibu ambazo zitafanyika nchi nzima kuanzia Machi Mosi, mwaka huu na madaktari kote nchi wataweka kambi sehemu tofauti tofauti na kutoa huduma za uchunguzi na matibabu bure.

Dk Osati alisema pia kutakua na semina ambayo itafanyika Machi 3 na itahusisha madaktari zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi na pia kupitia jarida la Tanzania Medical Journal watazungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na madaktari hapa nchini ili ziweze kuchapishwa na wananchi waweze kuzielewa.

MKUU wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza amesema Chama cha Skauti ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi