loader
Picha

ACT- Wazalendo waipongeza tume ya uchaguzi

Mawakala wa Chama cha ACT –Wazalendo katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wameipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kuendesha kwa uwazi, uadilifu na umakini kazi yauandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Mawakala hao wakizungumza kwa nyakati na vituo tofauti vyauandikishaji wapigakura katika Wilaya ya Micheweni, walisema wanaridhishwa na kazi hiyo.

Wakala wa Chama cha ACT –Wazalendo katika Kituo cha Wingwi Njuguni, Hamad Rashid Hamad, alisema uandikishaji unakwenda vizuri na wanapata ushirikiano mkubwa kutoka Tume ya Uchaguzi.

“Kituo kimefunguliwa mapema, saa 2:00 tumeanza kazi, hadi sasa hakuna matatizo mambo yanakwenda kama yalivyopangwa kama unavyoona mwenyewe” amesema Wakala huyo wa ACT-Wazalendo.

Katika Kituo cha Konde, Wakala wa Chama cha ACTWazalendo, Khamis Ali Khalid, alisema kwamba Tume imejipanga vizuri kuanzia vifaa vyauandikishaji, utaratibu wa uandikishaji na ushirikiano kwa mawakala.

Khamis Omar Idd, Wakala wa ACT-Wazalendo katika Kituo cha Tumbe Magharibi alisema uandikishaji unakwenda vizuri, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha katika kituo hicho.

Wakala wa Chama cha ACTWazalendo katika Kituo cha Micheweni, Elias Ameir alisema Tume ya Uchaguzi imefanya maandalizi mazuri, vifaa vya uhakika vya uandikishaji pamoja na kufunguliwa kwa wakati kituo hicho.

Hali kama hiyo pia imeelezwa na Wakala wa ACT-Wazalendo katika Kituo cha uandikishaji cha Shumba vyamboni, Khamis Mohammed Khamis akielezea kuridhishwa kwake na kazi yauandikishaji wapigakura katika daftari la kudumu.

Maelezo ya Mawakala hao yanaonekana kutofautiana na shutuma zilizotolewa na Viongozi wa ACT-Wazalendo Kisiwani Pemba. Mshauri wa ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad alidai kwamba kuna watu wengi wasiokuwa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na kudai kuwa wanaweza kukosa haki ya kujiandikisha, jambo ambalo Mawakala wa Chama chake wanalielezea tofauti.

Wilaya ya Micheweni kuna vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vimetekelezwa katika Ofisi za Wilaya za Wakala wa Usajili Matukio ya Kijamii Zanzibar licha ya kutolewa kwa matangazo mara kadhaa kuwataka wahusika wajitokeza kuvichukua,lakini hakuna aliyekwenda.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC) Jaji Hamid Mahmoud amepongeza watendaji wanaofanya kazi ya uandikishaji kwa kutumia teknolojia mpya ya uandikishaji inayorahisha wananchi kutekeleza haki yao ya demokrasia bila usumbufu.

Jaji Mahmoud alitoa pongezi hizo alipokuwa akitembelea vituo kadhaa vya uandikishaji na kuwahoji mawaka wa vyama vya siasa pamoja na waandikishaji ambao kwa pamoja walisema teknolojia hiyo ya kutumia mashine imerahishisha kazi yao na kufanya kutokuwapo makundi ya wananchi kwenye vituo.

MAMLAKA ya Maji ya Makonde iliyopo wilayani Newala mkoani Mtwara, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Pemba

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi