loader
Picha

CCM- Tutamng'oa Zitto kwa gharama yoyote

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema amedhamiria kuhakikisha analichukua Jimbo la Kigoma Mjini kwa gharama yoyote kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kumaliza utawala wa Mbunge wa jimbo hilo, Kabwe Zitto.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa viongozi wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Dk Bashiru amesema CCM imedhamiria kuhakikisha Mbunge huyo hapati ushindi kwenye nafasi yeyote atakayoomba katika uchaguzi mkuu ujao wa Rais, wabunge na madiwani na kusema kuwa mbinu iliyotumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo itatumika kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema kwa kiasi kikubwa yapo makosa ambayo yalichangia kumpa ushindi Mbunge huyo ikiwemo mivurugano ndani ya chama hasa iliyosababishwa na mchakato wa uchaguzi, mambo ambayo kwa sasa hayapo kwani CCM ni moja na viongozi na wanachama wake wameshikama kuhakikisha wanafanya kazi ya chama wakiwa pamoja.

Dk Bashiru amesema, fitina ndani ya chama ndiyo iligeuzwa kuwa siasa uchaguzi ukawa biashara na madalali wakaibuka ambapo bila pesa huwezi kupata nafasi ya uongozi, mambo hayo yalichangia kusalitiana na viongozi na wanachama wa CCM walifanya kampeni kwa upinzani ili kukomoana na ndiyo yaliyosababisha CCM kupoteza nafasi nyingi za ubunge na udiwani wakati huo.

“Tangu kuingia madarakani kwa Dk Magufuli (Rais John) mambo hayo yameanza kufanyiwa kazi na kurudisha imani kwa wananchi, tunataka viongozi wanaotumikia chama kwa uaminifu lakini watakaosimamia maendeleo ya wananchi ya wanaotaka kuingia kwa kujinufaisha binafasi,”alisema Katibu Mkuu wa CCM, Dk.Bashiru.

Katika Mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM amewataka wakuu wa wilaya nchini kote kutumia nafasi zao na mamlaka waliyonayo kuwachukulia hatua na kuwaweka ndani wagombea wote wa chama hicho watakaobainika kutumia vitisho na rushwa kupata uongozi.

Dk Bashiru akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma, alisema kuwa sifa pekee ya kiongozi atakayepata nafasi na kuteuliwa kugombea kwenye chama hicho ni zilizowekwa na chama na kukubalika na wananchi na wapiga kura na kwamba hakuna mgombea atakayewekwa kwa matakwa ya viongozi.

Pia Katibu huyo Mkuu wa CCM aliwataka viongozi waliohudhuria mkutano huo kutumia vikao kuibua na kubainisha vikwazo vya maendeleo na kuviwekea mkakati wa utekelezaji huku akiwataka watalaamu kutumia nafasi yao kukaa na wananchi katika kuibua na kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumzia tatizo la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa alisema jambo hilo lisiwagombanishe wananchi na serikali kwani Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inalifanya kazi.

MAMLAKA ya Maji ya Makonde iliyopo wilayani Newala mkoani Mtwara, ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Emanuel Lemburis
    20/01/2020

    Watanzani tuwe na Amani kwan mungu Ametubarik sisi na inchi yetu %% Ndomaana Neno linasema Heri Taifa Ambalo Bwana ni mungu wao

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi