loader
Picha

TLS yapendekeza viongozi miaka 3

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiomba viongozi wadumu madarakani miaka mitatu badala ya mwaka mmoja uliopendekezwa kwenye marekebisho ya sheria ya chama hicho kifungu namba 307.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuwasilisha mapendekezo mbele ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Rais wa TLS, Dk Rugemeleza Nshala alisema wanaomba uchaguzi wa viongozi wa juu wa chama hicho ufanyike kila baada ya miaka mitatu kutasaidia kupunguza gharama za kufanya uchaguzi kila baada ya mwaka.

Viongozi wa TLS walifika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria baada ya Bunge kutoa tangazo la kukaribisha maoni ya wadau kutoa maoni na mapendekezo kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 8 wa mwaka 2019.

Wadau mbalimbali wakiwemo TLS walifika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kutoa maoni yao kwa mujibu wa Kanuni ya 84 (20) ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari, 2016.

Rais wa TLS alisema chama hicho kilitoa maoni hayo, kikiomba muda wa utumishi wa viongozi wa juu wa chama uwe miaka mitatu ili kusaidia watendaji hao kupanga mipango na kutekeleza kwani mwaka mmoja ni mfupi.

Dk Nshala alisema wamefurahi mapendekezo ya marekebisho ya sheria hiyo kufutwa kwa kifungu kilichokuwa kinataka ifanyike mikutano miwili kwa mwaka na kubaki na mkutano mmoja.

Pia walipongeza mabadiliko hayo kuruhusu viongozi wa baraza kuu kugombea mara ya pili baada ya kumaliza muda wao, hata kama kwa uongozi wa miaka mitatu itakuwa vigumu kiongozi kugombea mara ya pili sababu ya ugumu wa kazi hiyo.

Dk Nshala aliomba kamati ikubali mapendekezo yao na kufanya mabadiliko ili mkutano mkuu wa chama hicho usiwe wa wawakilishi kutoka katika mikoa na kanda na jumuiya bali uwe wa mawakili wote.

Kifungu cha 21 kifungu kidogo cha 1-5 kimefanyiwa marekebisho na kuwa kifungu cha namba 57 (1-5) kinataka mkutano huo mkuu ukifanyika usihudhuriwe na mawakili wote bali uhudhuriwe na wawakilishi.

Kifungu hicho kinaonesha kwamba wawakilishi hao ni viongozi wa baraza, wajumbe wa kamati za kudumu kudumu, viongozi wa jumuiya wakiwakilisha mawakili vijana, wanawake, maveterani na wenye ulemavu, kamati tendaji za kanda, wajumbe wawili kutoka jumuiya waliochaguliwa na mkutano mkuu wa kanda na wengine watakaolikwa.

Dk Nchala alisema TLS inaomba kifungu hicho kifanywe mabadiliko ili kuruhusu mawakili wote kushiriki katika mkutano mkuu, badala ya wawakilishi, kwani kwa kufanya hivyo mikoa yenye mawakili wengi watakosa fursa hiyo inayopatikana mara moja kwa mwaka.

Ametoa mfano wa mkoa wa Dar es Salaam ambao una mawakili zaidi ya asilimia 75, hivyo kwa kuruhusu uwakilishi wengi wao watakosa haki ya kuhudhuria mkutano huo ukilinganisha na mikoa wenye mawakili wachache.

Dk Nshala alisema kifungu namba 57 (4) (a-g) kinachopendekeza aina ya uwakilishi kinapoka haki ya mawakili wengine kushiriki katika mkutano huo mkuu.

Alisema kwa kuweka mkutano wa uwakilishi, ipo siku itatokea watu wataunda vyama vya kikanda, hivyo ni vema mkutano huo ukabaki kuwa katika sura ya kitaifa kuliko kikanda.

Wakili Jebra Kambole alisema, chama hicho kilichoanza mwaka 1954 chenye wanachama zaidi ya 2,000 wakiwemo majaji na mahakimu, ni vema kila mwanachama akashiriki mkutano mkuu kuliko kuweka ushiriki wa kikanda.

MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amewashauri viongozi wanawake, ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi