loader
Picha

Maji yafunika mashamba Dodoma

WAKULIMA wa mpunga katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wamesema mashamba mengi yamefunikwa kwa maji huku mbegu za mpunga zikiharibiwa na nyingine kusombwa na maji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mmoja wa wakulima hao, Miraji Bakari alisema mashamba mengi ya mpunga yamefunikwa na maji baada ya mto Nkongwa kuhama na kuibua mikondo mingine.

Alisema maji mengi yamekuwa yakipita juu ya madaraja na kupelekea kumwaga maji mashambani.

"Kuna wakulima wengi mashamba yao yamefunikwa na maji wanashindwa kufanya kazi mpaka maji yatakapopungua, athari hiyo ni kubwa kwani mbegu nyingi za mpunga zimeharibiwa na nyingine kusombwa na maji," alisema.

Alisema majaruba yake 10 ya mpunga yamezama na amepata hasara kubwa kwani alikuwa ameshapanda mpunga na sasa anachosubiri na maji kupungua ili aweze kupandikiza tena mpunga.

Alisema mvua za mwaka huu zimekuwa nyingi lakini kuhama kwa mikondo ya mito kunakochangiwa na uharibifu wa mazingira na mito kujaa mchanga imewaletea sintofahamu kubwa kutokana na mvua kuendelea kunyesha.

Mkulima mwingine wa mpunga, Menas Muhumpa alisema "Mimi nilishapanda ila shamba langu liko kwa juu kwa hiyo hatujapata athari za maji kuzamisha mpunga lakini maeneo mengi mpunga umezama na mbegu kuchukuliwa na maji," alisema.

Alisema waliowahi kupanda mipunga imesaidia sana kwani mbua zinazonyesha zimekuta mpunga umeshashika," alisema.

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amevitaka ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Bahi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi