loader
Picha

Waziri- Wakandarasi Ruvuma wanaongoza wizi

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema wakandarasi wa Mkoa wa Ruvuma wanaongoza kwa vitendo vya wizi na udanganyifu wakati wa kutekeleza miradi ya maji.

Amesema wizi huo ni chanzo cha maeneo mengi katika mkoa huo kuendelea kukabiliwa na uhaba wa maji safi na salama licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo jana alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mkongo, Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani humo ulioanza kujengwa mwaka 2013 na mkandarasi Kampuni ya Kipera Contructor Co Ltd ya Songea, kwa gharama ya Sh bilioni 2.2 lakini hadi sasa bado haujakamilika.

Alisema vitendo vya wizi vinavyofanywa na wakandarasi kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya kata, halmashauri, mkoa na kutoka wizara ya maji ndiyo sababu ya miradi ya maji katika mkoa huo kushindwa kukamilika kwa muda muafaka, hivyo kuongeza tatizo la upatikanaji wa maji licha ya mkoa huo kuwa na vyanzo vingi vya maji.

Aidha,Waziri Mbarawa alibaini mapungufu mengi katika ujenzi wa mradi ikiwemo bei kubwa ya vifaa na uwezo mdogo wa Mkandarasi ambaye hadi sasa ameshalipwa Sh bilioni 1.3 kati ya Sh bilioni 2.2.

Baada ya kubaini tatizo hilo, Waziri Mbarawa amewaagiza mameneja wa Wakala wa Maji mjini na vijijini (Ruwasa) kote nchini kutowapa kazi ya ujenzi wa miradi ya maji wakandarasi wa Mkoa wa Ruvuma.

“Nasikitika Mkoa wa Ruvuma ndiyo unaoongoza kuwa na miradi mingi ya maji isiyokamilika kwa muda muafaka, jambo hili linatokana na wakandarasi wengi kutokuwa waaminifu, kila fedha ikiletwa wanachofikiria ni kuiba, badala ya kuwasaidia wananchi wenzao kuondokana na kero ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji,”alisema na kusisitiza:

“Kulikuwa na genge la wahuni wakiwemo viongozi, kazi yao ni kutafunafedha za maji tu kila zinapoletwa badala ya kusimamia ili zifanye kazi ya kuwaondolea maumivu Watanzania maskini”.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Mbarawa amekataa kuongeza muda wa ujenzi kwa mkandarasi na alisisitiza kuwa kazi zilizobaki zitafanywa na wahandisi wa Ruwasa badala ya kuendelea kuwatumia wakandarasi ambao wameonekana hawana uwezo.

Alisema, tayari wizara imeshatoa Sh milioni 110 ambazo zimetumika kununua mabomba na mwezi ujao serikali itatoa fedha nyingine itakayotumika kwa ajili ya kusambaza mabomba hayo.

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amevitaka ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Namtumbo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi