loader
Picha

Mtoto Dar aonesha dalili kupona saratani

MTOTO wa miaka minne, Ittai James mkazi wa Dar es Salam, aliyekuwa akiugua saratani ya tumbo ameonyesha dalili za kupona baada ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Narayana ya India, kumfanyia upandikizaji wa uroto.

Hospitali ya Muhimbili Mloganzil, Dar es Salaam itaanza kupandikiza uroto kwa wagonjwa wa saratani na wenye selimundu mwezi ujao.

Ittai alipandikizwa uruto Septemba, 2019 nchini India.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Narayana Health wa India Dk Sunil Bhat amesema Itanni alikuwa kwenye hatua ya mwisho ya ugonjwa huo lakini hospitali hiyo imefanikiwa kumpa tiba iliyoonesha mafanikio katika kipindi cha wiki tatu.

Baba mzazi wa mtoto huyo James Moshi ambaye ni mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) amesema alimpeleka mwanawe Bengaluru, India mwishoni mwa mwaka 2018 kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na homa kali, mwili kumuuma na maumivu ya tumbo.

“Hakuna matibabu yaliyomsaidia licha ya kwenda kwenye hospitali tofauti tofauti hapa nchini, Oktoba 2018 hakuweza hata kutembea,”amesema Moshi.

Amesema hospitali hiyo ya Narayana kwa mara ya kwanza ilianza kumtibu maambukizi ya bakteria yaliyosambaa hadi katika mifupa na ndipo jopo la madaktari wakaamua kumfanyia vipimo vikubwa vya uchunguzi na akabainika na saratani.

“Tulipata taarifa kuwa hospitali ya Narayana ina uwezo wa kutibu saratani hii. Nina furaha kumuona mwanangu kwa sasa anacheza na anafurahi,” amesema mama mzazi wa mtoto huyo Scholastica Musokwa.

Akizungumzia upasuaji wa mtoto huyo kabla ya kumpandikiza uruto Dk Bhat amesema walimuondoa uvimbe uliokuwa na dalili za saratani Julai 2019 na Septemba mwaka jana na wakampandikiza seli za damu kutoka kwenye uroto wa mwilini mwake.

Naibu Mkurugenzi wa Muhimbili, Julieth Magandi amesema kuanza kutolewa kwa huduma hiyo nchini itasaidia kutibu wanachi wengi zaidi hasa wenye saratani.

Kuhusu gharama amesema wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi ni Sh milioni 200 kwa anayepandikizwa uroto kutoka kwa ndugu yake, wakati kwa anayepandikizwa wa kwake mwenyewe hugharimu hadi Sh milioni 150.

“Kwa mwaka, watu 130 hadi 150 wanahitaji huduma hii na theluthi mbili ya wagonjwa hufariki dunia kila mwaka kwa kukosa huduma hiyo ambayo gharama yake ni kubwa”amesema.

Magandi amesema utoaji wa huduma hiyo nchini utapunguza idadi ya vifo na pia itaipunguzia serikali gharama ya kupeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

Pia gharama za tiba zitapungua kwa asilimia 50 kutoka kwenye gharama za kutibia nje ya nchi hivyo Muhimbili imejipanga kuhudumia wagonjwa wote wa ndani na nje ya nchi watakaokuja kutibiwa kuanzia mwezi ujao yaani February.

Dk Magandi amesema kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, huduma hiyo itakuwa ikipatikana Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na Muhimbili Upanga ambako vipimo vyote vitakua vikipatikana hapo wakati matibabu ni Mloganzila pekee na hivyo hospitali hiyo imejipanga kuwahudumia pia wagonjwa kutoka nchi za jirani.

Kwa mujibu wa Dk Magandi huduma hiyo ya uroto ni ya kupandikiza chembechembe mama za kuzalisha damu, ambazo hupatikana kwenye uroto au kutoka kwenye chembechembe mama kwenye kitovu cha mtoto mchanga au kondo la nyuma la mama.

Amesema njia inayotumika zaidi ni ya kupandikiza chembechembe mama za damu kutokea kwenye uroto itawasaidi wagonjwa wote wanaopatwa na changamoto ya damu hasa zitokanazo na saratani.

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro amevitaka ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi