loader
Picha

Magufuli ataja vipaumbele 2020

Rais John Magufuli amesema, Serikali imejipanga kuendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano mwaka huu.

Ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2020.

"Kipaumbele chetu itakuwa kuendelea kudumisha amani na kuimarisha muungano wetu. Vipaumbelea vingine vitakuwa ni kukuza uchumi ambapo tunalenga uchumi ukue kwa asilimia 7.1, kudhibiti mfumo wa bei ili usizidi asilimia tano" amesema.

Dk Magufuli amesema pia kuwa Serikali itaimarisha akiba ya fedha za kigeni, itaongeza ukusanyaji wa mapato na kukuza sekta za uchumi na uzalishaji kwenye viwanda, ujenzi na utalii.

"Lakini pia kuruhusu wafanyabiashara na kukuza sekta ya biashara ya watu mbalimbali nchini na kutoka duniani kote kwa ajili ya uwekezaji katika biashara watakazochagua wao" amesema.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji, na kwamba, Julai mwaka jana Serikali ilianza kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira hayo.

"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba mabalozi kuwashawishi wafanyabiashara kutoka kwenye nchi zenu kuja kuwekeza hapa Tanzania. Tanzania ni mahali pazuri pa kufanya biashara"amesema.

JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi