loader
Picha

Naibu Waziri- Chips zitamaliza nguvu za kiume

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amesema miaka 50 ijayo wanaume watakosa nguvu za kiume kutokana na mabadiliko ya tabianchi na vyakula wanavyokula ikiwamo chipsi.

Alitoa kauli hiyo jijini hapa wakati akijibu hoja za wabunge wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ilipokutana na Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zake. Alisema tafiti za kidunia zinaonesha katika miaka 50 kuna upungufu nguvu za kiume kwa asilimia 50.

“Kuna utafiti mmoja unaonesha kuwa katika miaka 50 ijayo wanaume wote tutakuwa hamna kitu na visababishi ni mabadiliko ya hali ya hewa na maisha tunayoishi,”alisema Ndugulile.

Alisema aina ya maisha ambayo watu wanaishi sasa na vyakula vinavyoliwa ikiwemo chipsi yanasababisha tatizo hilo hivyo kutaka waache.

Alisema ugumba imekuwa ni tatizo kubwa nchini na Hospitali ya Muhimbili imeshaanza maandalizi ya kuanzisha kutoa huduma hiyo.

“Tunatambua hospitali za binafsi zinafanyia kazi jambo hili. Tunataka kwa upande wa serikali na sisi tuanze kutoa huduma,”alisema.

Mbunge wa Viti maalum, Susan Lyimo (Chadema) alitaka kujua serikali imejipangaje kuimarisha huduma ya kuzibua mirija ya uzazi na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tatizo hilo.

“Tatizo la wanawake kushindwa kupata watoto kwa wakati limekuwa likichangia ndoa nyngi kuvunjika kwa miaka ya hivi karibuni,”alisema.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia vituo vya huduma za afya. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara Julai hadi Desemba 2019, Ummy alisema malengo yalikuwa kipindi hicho wajawazito milioni 1.1 wakajifungulie vituo vya afya.

“Matarajio yalikuwa ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua kipindi cha miezi sita, hata hivyo takwimu zinaonesha wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 walijifungua

MISIKITI ya Zanzibar imeanza kutekeleza agizo la Mufti wa Zanzibar ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

1 Comments

  • avatar
    Paul luziga
    22/01/2020

    Ni kweli kabisa lakini serikali haijawekeza vya kutosha ili kuondokana na tatizo hill inasubiri liwe zito ndipo waje na mkakati wa zima moto.kama chanzo wanakijua kwanini wasichukue hatua.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi