loader
Picha

U17 kuikabili Burundi leo

TIMU ya Taifa ya Soka ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17, leo inashuka uwanjani kucheza mchezo wa marudioano kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India dhidi ya Burundi, utakaochezwa Bujumbura katika Uwanja wa Intwari, (zamani Prince Louis Rwagasore).

Timu hiyo ambayo iliondoka juzi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ikiwa na wachezaji 17, inapewa nafasi ya kushinda mchezo huo baada ya mchezo wa awali kushinda kwa mabao 5-1 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana kwa njia ya mtandao, Kocha wa timu hiyo Bakari Shime alisema wanajua mchezo huo utakuwa mgumu, lakini wamejiandaa kisaikolojia na kimbinu kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

“Tunajua mchezo dhidi ya Burundi utakuwa na ushindani kwani tunafahamiana vizuri, hivyo tumejiandaa kuhakikisha tunaendeleza rekodi ya kuwafunga ili tufuzu hatua inayofuata japo tunajua watacheza kufa au kupona mbele ya mashabiki wao,” alisema Shime.

Shime alisema anashukuru walifika salama na jana wamefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja watakaocheza, na hakuna majeruhi. Naye nahodha wa timu hiyo, Irene Kisisa alisema wamejiandaa vizuri na wana kila sababu ya kushinda mchezo huo huku akiwataka Watanzania kuwaombea.

“Tumejiandaa vizuri, hivyo tunaamini tutapata ushindi katika mchezo ujao ili tusonge mbele, tunamshukuru Mungu tayari tuna akiba ya mabao manne, Watanzania wazidi kutuombea,” alisema Irene. Endapo Tanzania itashinda mchezo huo itakutana na mshindi kati ya Uganda na Ethiopia.

MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog, ametangaza kuwa, atachangia Dola za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi