loader
Picha

Taekwondo kufanya onesho Zanzibar

CHAMA Cha Taekwon-do ITF leo kinatarajiwa kufanya onesho maalumu la mchezo huo kwa lengo la kuutangaza kwa jamii.

Onesho hilo ambalo linaenda sambamba na ufunguzi wa klabu mpya ya mchezo huo litafanyika katika viwanja vya Mao Dze Dong saa 3:00 asubuhi.

Akizungumza jana kuhusu hafla hiyo, Katibu wa chama hicho, Rashid Hamad alisema onesho hilo ni la wazi na wananchi wote wanakaribishwa ili kuja kuona mchezo huo.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa wana lengo la kutangaza lakini pia wanataka kuionesha jamii juu ya utofauti wa mchezo huo na sanaa nyingine.

Alisema kuwa baada ya kuzindua klabu hiyo kutakuwa na mwendelezo wa kufanya mazoezi ndani ya uwanja huo kwa siku za Jumanne, Alhamis na Ijumaa wakati wa saa 10:30 alasiri na Jumamosi saa 1:30 hado saa 3:00 asubuhi, na wale wanaotaka kujiunga wanakaribishwa.

Ofisa Habari wa chama hicho, Ahmed Rashid Salami aliishukuru Serikali kwa kuwapatia uwanja huo bure kuweza kufanya mazoezi kwa siku ambazo zimetajwa hapo juu

MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog, ametangaza kuwa, atachangia Dola za ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi