loader
Picha

Klabu 15 kupambana vishale Arusha

KLABU 15 kutoka mikoa mitatu zinatarajiwa kushiriki mashindano ya mchezo wa vishale yanayotarajiwa kutimua vumbi jijini hapa kuanzia leo na kesho katika ukumbi wa Magereza.

Mkoa Arusha utawakilishwa na klabu 12, Kilimanjaro klabu tatu, klabu moja kutoka wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Akizungumza jana Katibu Mipango wa Chama cha Vishale Mkoa Arusha (ARDA), Jackson Vitus alisema michuano hiyo itafanyika ikiwa na lengo la kukuza, kuinua mchezo na kuongeza hamasa ya mchezo huo .

Alisema kwa mwaka 2019/2020 mwitikio wa klabu za vishale ni mkubwa na nyingine mpya zimeanzishwa.

“Bado hakuna ufadhili licha ya kuongea na kampuni kadhaa kuomba zituunge mkono, lakini imeshindikana kutokana na hali nya uchumi na kusema wanaendelea kuwaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia, ”alisema Vitus.

Katibu wa Chama cha Vishale Tanzania (TADA), Victor Kimambo alisema mkoa wa Arusha umeamka, kwani klabu zinaongezeka pia Kilimanjaro nao wanaonyesha nia na michuano hiyo hivyo ni moja ya njia katika kukuza mchezo huu.

“Kulingana na kalenda ya TADA tumesisitiza mikoa yote itengeneze kalenda zao za mwaka na kwa mkoa wa Arusha tayari wameainisha, hivyo mikoa yote inatakiwa ianze mchujo wa wachezaji kwa ngazi ya klabu, wilaya mkoa kwenda kanda kuelekea michezo itakayofanyika mwezi Mei mkoani Dodoma kuunda timu ya taifa,” alisema Kimambo.

Alieleza nia yao ni kukuza mchezo huo, hivyo viongozi wote wana jukumu la kuhakiksha wanakuwa mstari wa mbele kuamsha

MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog, ametangaza kuwa, atachangia Dola za ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi