loader
Picha

 Waziri Mkuu aipongeza Geita usimamizi mzuri sekta ya madini

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel kutokana na kusimamia vyema michango inayotolewa na Kampuni ya Madini ya Geita (GGM) kwa ajili ya shughuli za kijamii mkoani huko.

Waziri Mkuu aameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifunga rasmi Semina ya siku mbili iliyoshirikisha Wizara ya Madini, Vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mikoa yote nchini pamoja na wadau wa madini iliyolenga katika kuimarisha usimamizi na udhibiti wa rasilimali madini.

Akizungumza kuhusu uwajibikaji wa kampuni za madini kwa jamii, Majaliwa alimpongeza Mkuu huyo wa mkoa kwa kusimamia vyema Sh Bilioni 10 zilizotolewa na GGM kwa ajili ya kuwezesha maendeleo ya kijamii mkoani humo ikiwemo ujenzi wa zahanati huku akiwataka watendaji wengine wa Serikali kuiga mfano huo.

Waziri Mkuu pia ameipongeza Wizara ya Madini kutokana na kusimamia sekta ya madini  kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta na kuzifanyia kazi ikiwemo usimamizi wa ukusanyaji mapato na kueleza kuwa imekuwa mfano mzuri katika kuongeza tija na kwamba matokeo yanaonekana.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko amemweleza Waziri Mkuu kuwa bado ipo changamoto ya madini bandia ambayo baadhi ya watanzania ambao kwa kutumia viwanda vyao wamekuwa wakitengeneza madini hayo na kuwaeleza kuwa, “Serikali itaweka mkakati maalum kuhakikisha suala hilo halifanyiki Tanzania...

“…Mheshimiwa Waziri Mkuu zama za biashara ya haramu na madini bandia sasa ni zilipendwa, kwa kushirikiana na vyombo hivi tutahakikisha madini hayo zama za biashara haramu  zinakwisha nchini,” alisisitiza Waziri Mkuu.

 

SHULE ya Msingi Kawe B, Dar es Salaam imeahidi kufanya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi