loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shein ala chakula na vijana wa halaiki

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameungana na vijana wa halaiki na wahamasishaji, walioshiriki katika maadhimisho ya sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chakula maalum alichowaandalia.

Aliwaandalia chakula hicho kutokana na ushiriki wao kwenye sherehe hizo zilizofanyika Januari 12 mwaka huu katika Uwanja wa Amani mjini Unguja.

Hafla ya jana ilifanyika katika Viwanja vya Polisi Ziwani na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma.

Wengine ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, mawaziri, naibu mawaziri na washauri wa Rais wa Zanzibar. Katika shukrani za Rais kwa vijana hao, zilizotolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi ‘Gavu’, alisema Rais Shein ana imani kubwa kuwa vijana hao watakuwa sehemu ya ulinzi wa taifa hilo kutokana na kujitoa kwao na uzalendo waliouonesha.

Alisema katika kipindi chote cha maandalizi ya sherehe hizo, vijana hao walikuwa wakipokea vyema maelekezo wanayopewa na viongozi wao na kuyafanyia kazi kwa maslahi ya taifa.

Alimpongeza Dk. Shein kwa uongozi wake madhubuti, uliowezesha kuwepo kwa amani na utulivu, umoja na mshikamano. Alisema uongozi wake umesaidia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi hapa nchini.

Katibu wa Halaiki na Uhamasishaji, Ali Mohamed Baraka alitoa shukurani za dhati kwa Rais Dk. Shein kwa mwaliko huo na kutoa ahadi ya vijana hao kuendelea kushirikiana na serikali ili kufanikisha vyema shughuli zinazoandaliwa.

UZALISHAJI wa chakula umeimarika na hivyo kuwezesha nchi kujitosheleza kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi