loader
Picha

Mikutano isiyofuata taratibu itaendelea kuzuiwa - Masauni

NAIBU wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amezungumza hali ya usalama visiwani Zanzibar, akisema imeimarika. Alisisitiza kuwa msimamo wa kuzuia mikutano yote ya siasa isiyofuata utaratibu, upo palepale.

Katika maelezo yake, Masauni alisema muda wa siasa ukifika, watu wataruhusiwa kuendesha mikutano mbalimbali yenye lengo la kueleza kwa wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa nafasi, baada ya kuchaguliwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali.

Alieleza hayo wakati akitoa taarifa ya usalama na uhalifu visiwani Zanzibar, katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana katika mahojiano na kituo kimoja cha redio.

Katika mazungumzo hayo, Masauni alianza kuzungumzia mauaji, ambapo alisema mwaka 2018 jumla ya matukio 40 ya mauaji yalitokea, tofauti na mwaka jana ambapo matukio hayo yalikuwa 35. Alisema kazi kubwa imefanyika kupunguza matukio hayo hadi kufikia idadi hiyo.

Alisema serikali kupitia jeshi la polisi na pande zote zinazohusika, zimeanza harakati kuweza kudhibiti matukio hayo yanayosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina.

Matukio ya udhalilishaji Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2019, matukio ya udhalilishaji yalionekana kuongezeka tofauti na mwaka 2018, ambapo matukio 15 yaliripotiwa.

Sababu za vitendo hivyo alitaja kuwa ni imani za kishirikina, jamii kukosa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya makosa hayo, watu kushindwa kuzuia matamanio, ukuaji wa matumizi ya mitandao, kutotolewa adhabu stahiki na kwa muda muafaka kwa wakosaji na kuwepo mmomonyoko wa maadili.

MKUU wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza amesema Chama cha Skauti ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi