loader
Picha

Uchafu Soko la Sabasaba wamkera Waziri Jafo

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amekerwa na hali ya uchafu katika Soko la Sabasaba. Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kulifanyia ukarabati soko hilo haraka.

Jafo alioneshwa kukerwa na hali hiyo, baada ya kujionea uchafu uliokithiri na mifereji ya kupitisha maji ya mvua, ikiwa imejaa uchafu katika eneo la soko wakati alipofanya ziara ya kikazi juzi.

Kutokana na hali hiyo, Jafo aliagiza uongozi wa jiji kuhakikisha soko hilo, linakuwa safi na kufanya ukarabati wa haraka ili kuwalinda wafanyabiashara na wananchi.

“Najua Jiji la Dodoma halina mashaka katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, na najua mnafanya mambo makubwa na mazuri lakini kwa hili la soko la Sabasaba hapana, sijaridhishwa na hali ya soko na ni vyema mkalifanyika kazi kwa haraka”alisema.

Jafo aliongeza: “Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma sijafurahishwa na hali ya uchafu uliopo katika soko hili, uchafu huu unahatarisha afya za wafanyabishara na wananchi kwa ujumla, nakuagiza kuhakikisha soko hili linafanyiwa ukarabati.

“Wafanyabishara hawa ndio wapiga kura wa Rais Dk John Magufuli, hivyo wanatakiwa kufanya biashara zao katika mazingira mazuri na masafi na si katika mazingira kama haya ya kuwapo kwa uchafu uliokithiri.”

Alisema jambo la kushangaza ni kwa uongozi wa jiji, kushindwa kuweka mazingira mazuri kwenye soko hilo wakati Jiji la Dodoma lina uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ya zaidi ya Sh bilioni 70.

Aidha, Jafo aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kusimamia usafi na kuhakikisha mitaro inasafishwa ili kulinda afya na usalama wa wafanyabishara na wananchi.

Hivi karibuni, Jafo pia alitoa wiki mbili kwa uongozi wa jiji hilo, kuhakikisha vifaa vinavyotumika katika mchakato wa usidiliaji wa taka katika dampo la kisasa, vinafanya kazi kwa asilimia 100, ili dampo hilo lirudi katika uwezo wake wa kufanya kazi.

Alitoa agizo hilo baada ya kubaini mitambo miwili kati ya minne inayofanya kazi kwenye dampo hilo kuharibika, hivyo kufanya usambazaji na ushindiliaji wa taka, kutofanyika vizuri.

JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi