loader
Picha

Wafurahia kupima HIV bila ridhaa ya wazazi

MTANDAO wa Watoto na Vijana nchini, umeipongeza Serikali kufanyia marekibisho Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi ya mwaka 2008 ili kuruhusu vijana kuanzia miaka 15 kupima Ukimwi bila ridhaa ya wazazi au walezi. Lakini, pia wameiomba Serikali kufanyia marekebisho kanuni na miongozo ili iende sambamba na mabadiliko ya sheria hiyo.

Wakizungumza Jijini hapa mwishoni mwa wiki, Viongozi wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mwanza (MYCN), ulioenea nchi nzima, pia waliiomba serikali kuwapa nafasi watoto na vijana, washiriki katika mchakato huo wa uhuishaji kanuni na miongozo hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Tanzania, Aidath Ishulula alisema licha ya Sheria ya Ukimwi kufanyiwa marekebisho, kutokuwepo kwa kanuni na miongozo, inayosimamia upimaji wa VVU kwa vijana kuanzia miaka 15, kumekwamisha vijana wengi kujitokeza kupima.

“Tunaiomba serikali kufanyia marekebisho kanuni na miongozo ya upimaji VVU ili iende sambamba na mabadiliko ya Sheria ya Ukimwi hususani katika upimaji wa vijana kuanzia miaka 15 bila ridhaa ya wazazi au walevi,” alisema Ishulula.

Alisema uwepo wa kanuni na miongozo, inayoendana na sheria, utasaidia pia watoa huduma za upimaji wa VVU kuwapima vijana na watoto, kwa kuzingatia miongozo na kanuni zinazoakisi mabadiliko ya sheria ya Ukimwi. “Pia itasaidia vijana na watoto wengi kujitokeza kupima VVU na kujua afya zao na kisha kuanza matibabu kwa wale watakaokuwa na maambukizi na kwa wale ambao hatakuwa na maambukizi wajilinde zaidi,” alisema.

Ishulula aliomba serikali mara itakapoanza mchakato wa marekebisho ya kanuni na miongozo, basi iwashirikishe vijana na watoto kikamifilifu ili kuwa na kanuni na miongozo ya upimaji Ukimwi rafiki kwao.

Mwakilishi wa Vijana Mkoa wa Shinyanga, Rashid Omary alisema vijana na watoto kutoka mikoa sita nchini ya Dodoma, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Shinyanga na Tabora na wawakilishi wa wengine nchini, wanaiomba serikali iwape nafasi ya kushiriki katika marekebisho ya kanuni na miongozo ya upimaji VVU kwa vijana kuanzia miaka 15.

Alisema hali ya maambukizi ni asilimia 43 ya watu 222 ambao ni sawa na vijana 96 kila siku ambao huambukizwa VVU nchini. Hali hiyo inaashiria kwamba vijana wa umri kati ya miaka 15-24, ndilo kundi ambalo lipo katika hatari kubwa ya kupata VVU kuliko kundi lingine lolote nchini, hivyo ni vema washiriki katika mchakato ili kuhamasisha vijana kupima na kujua afya zao.

Mhamasishaji wa Vijana Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Nchini, Doreen Odemba alipongeza serikali kwa kuwashirikisha katika mchakato wa kufanyia marekebisho Sheria ya Ukimwi ya mwaka 2008 hususani Kifungu 15 (2) kilichokuwa kinazuia watoto chini ya miaka 18 kupima VVU bila ridhaa ya wazazi au walezi.

“Tunaipongeza serikali kwa kusikiliza kilio chetu na kuifanyia marekebisho sheria hii na kuruhusu vijana na watoto wenye umri kuanzia miaka 15 kupima bila ruhusa kutoka kwa wazazi au walezi,” alisema Odemba.

Alisema wanaoimba iharakishe mchakato wa kufanya mabadiliko ya kanuni na miongozo ili kusaidia kutimiza malengo ya kidunia ya 90-90-90 na lengo la nchi yetu la kuwa na Tanzania isiyokuwa na VVU/Ukimwi.

JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi