loader
Picha

Mwaluko atamba kumaliza kero sugu ya ardhi Chinyoyo

DIWANI wa Kata ya Kilimani Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Neema Mwaluko (CCM) amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kata kwa kipindi cha miaka minne.

Amesema ameweza kushughulikia tatizo la ardhi katika eneo la Chinyoyo, lililodumu kwa miaka 20.

Kata ya Kilimani ambayo ni miongoni mwa kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ina mitaa minne na jumla ya wakazi 6,831.

“Nimeshughulikia tatizo la ardhi kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, nimefanikiwa kutatua kero kubwa ya upimaji wa mtaa wa Chinyoyo iliyodumu takribani miaka 20, sasa mtaa umeshapimwa kwa njia ya maboresho kila mtu atabaki pale alipojenga tupo katika hatua ya mwisho ya maboresho kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa Jiji,” alisema.

Pia, alisema katika uwezeshaji wananchi kiuchumi, amehamasisha na kutoa elimu ya namna bora ya kukuza biashara na kuziboresha, uundaji wa vikundi na jinsi ya upatikanaji wa mikopo inayotolewa na halmashauri. Alisema katika kipindi cha miaka minne, vikundi 43 viliundwa na kukaguliwa na kupatiwa usajili.

Alisema vikundi 18 vilipatiwa mikopo ya halmashauri ya Sh 65,129,500. Alisema wamefanikiwa kutenga eneo la kujenga soko mtaa wa Chinyoyo, lenye ukubwa wa mita za mraba 5,518.

Kwamba soko hilo litafanya mzunguko wa fedha kuwa mkubwa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali. Alisema kata hiyo ni miongoni mwa kata zinazopokea huduma ya kunusuru kaya maskini chini ya TASAF. Kuna jumla ya walengwa 113 na fedha walizopatiwa mpaka sasa ni Sh ilioni 89.4.

Alisema mtaa wa Chinyoyo una walengwa 80, mtaa wa Nyerere walengwa 11, Imagi walengwa 11 na Kilimani walengwa 11.

“Kupitia mradi wa Tasaf tumefanikiwa kuwapatia walengwa elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya uundaji wa vikundi vya uzalishaji mali ambapo hadi sasa vimekwishaundwa vikundi vine na vimesajiliwa.

SHULE ya Msingi Kawe B, Dar es Salaam imeahidi kufanya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi