loader
Picha

Wakandarasi wahimizwa kuzingatia viwango

BODI ya Makandarasi nchini (CRB), imesema kama makandarasi wazalendo watakamilisha miradi ya ujenzi wanayopewa kwa viwango vinavyokubalika na kwa wakati, serikali itawapa zabuni za miradi mingi na mikubwa kama sehemu ya kuendelea kuwaimarisha.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki mjini Arusha na Msajili wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Rhoben Nkori, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wakandarasi na wamiliki wa kampuni za ujenzi nchini.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa wakandarasi wazalendo serikali sasa imeweka mpango kwamba wakandarasi kutoka nje ya nchi wakija nchini kufanya kazi za ujenzi wa miradi lazima washirikiane na wakandarasi wazawa hivyo alisema hiyo ni fursa kwao kufanya vizuri. Aliwataka wakandarasi kuwa waaminifu, washirikiane na kuwa na mawasiliano mazuri wanapopewa kandarasi za ujenzi kama njia moja ya kufikia maendeleo waliyojiwekea. “Kuna wakandarasi wazuri katika kazi na wanapata zabuni nyingi, lakini hawamalizi kazi kwa wakati hivyo wanawaharibia wengine kukosa kazi kwasababu wanaonekana ni wale wale tu hivyo boresheni kazi zenu na mkipewa kazi mkamilishe kwa wakati,” aliongeza. “Unaweza kukosea jambo dogo likasababisha ukose kandarasi nyingine, hivyo tunaomba wanaopata kandarasi watekeleze kwa wakati na kwa ubora ulioainishwa kwenye mikataba mnayoandikishiana na wateja wenu,”alisema.

Aliwataka makandarasi nchini kutumia mafunzo yanayotolewa na bodi ya wakandarasi kuleta mabadiliko chanya katika kampuni zao za ujenzi kwa kufanya kazi kwa ubora.

Alisema kama wakandarasi hao, watatumia vizuri mafunzo hayo, kampuni zao zitakuwa za ushindani mkubwa katika kutafuta kandarasi za ujenzi wa miradi mikubwa na ile midogo.

“Mafunzo haya mkayazingatie na kuyafanya kazi kwa vitendo katika utekelezaji wa miradi kwenye makani yenu ya ujenzi,”alisema.

Licha ya kuzungumza hayo, Nkori aliwataka wakandarasi hao kuwasimamia vizuri wafanyakazi wao na kila mmojawapo awajibike kulingana na nafasi yake ili miradi wanayopewa waifanye kwa ufanisi mkubwa.

JESHI la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi