loader
Picha

Ofisa mtendaji atuhumiwa kumbaka mwanafunzi

Ofi sa Mtendaji wa Kijiji cha Mirumba katika Kata ya Kibaoni wilayani Mlele, Ignas Katula anatuhumiwa kumbaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda.

Gazeti hili lilimpiga simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzanga ambaye alijibu kupitia ujumbe mfupi wa maneno kuwa yupo kikaoni.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Kituo cha Polisi Kibaoni, zinadai mtuhumiwa huyo alishikiliwa kwa saa 12 kituoni hapo kuhusiana na tuhuma hzio.

“Mie sio msemaji wa jeshi hili lakini ni kweli mtuhumiwa huyo alikamatwa na kushikiliwa kwa zaidi ya saa 12 kituoni hapa kisha akaachiwa kwa dhamana, siwezi kueleza kwa kina,”alisema mtoaji taarifa.

Akizungumza na gazeti hili, Diwani wa Kata ya Kibaoni, Wilbroard Mayala alikiri kuzagaa kwa taarifa hizo huku akithibitisha kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na kushikiliwa kwa muda na jeshi la polisi kisha akaachiwa kwa dhamana.

“Taarifa za mtuhumiwa huyo kutuhumiwa kumpatia ujauzito zipo na zimezagaa sana, ni vigumu kuthibitisha kama ni kweli ametenda uhalifu huo au la, ila ninachofahamu ni kwamba kukamatwa na kushikiliwa kwa mahojiano na jeshi la polisi kwa muda lakini ameachiwa kwa dhamana,”alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mirumba, Japhet Bundara akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema atatoa maelezo ya kina leo akifika ofini kwake huku akisisitiza kuwa taarifa za tukio hilo ni tetesi tu zilizomfikia.

SHULE ya Msingi Kawe B, Dar es Salaam imeahidi kufanya ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi