loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Trump, Messi, Ronaldo wamlilia Bryant

WATU mashuhuri, wanamichezo nyota na wanasiasa wametuma salamu za rambirambi kwa kifo cha gwiji wa mchezo wa mpira wa kikapu duniani, Kobe Bryant aliyefariki dunia Jumapili asubuhi kwa ajali ya helkopta.

Katika ajali hiyo, Bryant alifariki dunia na mtoto wake, Gianna na watu wengine tisa waliokuwemo ndani ya helkopta hiyo.

DONALD TRUMP

Rais wa Marekani, Donald Trump ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mchezaji huyo wazamani. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump aliziita taarifa za kifo cha mchezaji huyo kuwa ni “mbaya” na za kusikitisha.

BARACK OBAMA

Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama naye amemlilia mchezaji huyo mashuhuri akisema kuwa, kifo cha Bryant pamoja na mtoto wake ni pigo kubwa. Obama katika taarifa yake alisema kuwa, Kobe alikuwa gwiji uwanjani, ni pigo kubwa kwa kifo chake.

Kumpoteza Gianna pia ni pigo kubwa kwetu kama wazazi. Mimi na mke wangu (Michelle) tunatuma salamu za rambirambi kwa wachezaji, Vanessa na familia nzima ya Bryant katika siku hii isiyo fikirika.

MESSI, RONALDO

Wachezaji nyota wa michezo mbalimbali nao hawakuwa nyuma kumlilia nyota, mmoja ni mchezaji golfu maarufu Tiger Woods, bingwa mara 15 wa mashindano makubwa, anasema alisikia taarifa za kifo cha Bryant wakati akikamilisha raundi ya mwisho ya mashindano ya Farmers Insurance Open, California.

LIONEL MESSI

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi aliandika katika ukurasa wake wa Instagram: “Sina cha kusema ... Mapenzi yangu yote ni kwa familia ya Kobe na marafiki zake. Lilikuwa jambo zuri kukutana nawe na kubadilishana mawazo. Ni mtu wa aina yake,” alisema.

CRISTIANO RONALDO

Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo alisema taarifa hizo ni za kuhuzunisha sana, aliongeza Bryant alikuwa gwiji kweli na mfano kwa wengine wengi, naye kiungo wa Manchester United Paul Pogba aliongeza:

“Mashujaa huja na kuondoka, lakini magwiji wako milele.” Muingereza bingwa mara sita wa mbio za magari za Formula 1, Lewis Hamilton alisema:

“Nina huzuni kubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wakubwa, ambaye alikuwa mfano kwa wengi, nikiwemo mimi.”Mshambuliaji wa Brazil na Paris St-Germain (PSG), Neymar alitoa salamu za rambirambi kwa kushangilia baada ya kufunga bao Jumapili walipocheza dhidi ya Lille.

Baada ya kufunga bao la pili kwa penalti, aliinua vidole viwili katika mkono mmoja na vinne mkono mwingine, akimaanisha namba 24 ya jezi aliyokuwa akiivaa Bryant wakati akiichezea Lakers.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, ni shabiki mkubwa wa mpira wa kikapu ambaye aliwahi kukutana na Bryant, ambaye pia alionesha ishara ya kifole kimoja angani.

RAFAEL NADAL

Bingwa namba moja wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal alitweet:

“Niliamka asubuhi hii na kukutana na taarifa za kusikitika za kifo cha mmoja ya wachezaji wakubwa duniani, Kobe Bryant, na mtoto wake Gianna na abiria wengine. Rambirambi zangu ziende kwa mke wake na familia yake kwa ujumla, kwa kweli nimeshtushwa sana.”

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi