loader
Dstv Habarileo  Mobile
Uwanja fainali ya FA unahitaji marekebisho

Uwanja fainali ya FA unahitaji marekebisho

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka viongozi wa Mkoa wa Rukwa kusimamia Uwanja wa Nelson Mandela unaofanyiwa marekebisho ili uwe tayari kwa mchezo wa fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Hayo yalisema na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF jana, Salum Madadi baada ya kutembelea na kukagua uwanja huo juzi na kujiridhisha kuwa unahitaji marekebisho hasa sehemu ya kuchezea.

“Uwanja wa Nelson Mandela unahitaji kufanyiwa matengenezo muhimu kwa sababu haujawahi kutumika kwa mashindano makubwa, pia ili uendane na viwango vinavyotakiwa na CAF na FIFA,” alisema Madadi.

Pia Madadi alisema TFF inatoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa ulivyojipanga katika maandalizi ya fainali hizo. Katibu Tawali wa Rukwa, Makali aliihakikishia TFF kuwa Mkoa wa Rukwa umepokea kwa dhati kuwa mwenyeji wa fainali hizi za 2020 na kumhakikishia kufanya marekebisho kwa sehemu zote zilizotakiwa kurekebisha. “Fainali hizi ni kubwa, tuko tayari, tumeanza maandalizi .

Tunawaasa wananchi na wadau wa michezo kutoa ushirikiano kuanzia sasa ajenda yetu ni hii ili fainali zifanyike kwa ufanisi mkubwa,” alisisitiza Naye Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Sumbawanga, Jacob Mtalitinya alisema mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Rukwa na kuwataka wakazi wake kuchangamkia fursa hiyo.

“Kutakuwa na wageni wengi kutoka mikoa ya jirani hata nchi jirani ...pia timu mbili zitakazocheza fainali watakuwa na wachezaji na viongozi wao ambao watalala mjini hapa. Hivyo nawashauri wafanyabishara wenye nyumba za kulala wageni na wajasiriamali kuchangamkia fursa hii,” alisisitiza.

TFF ilitangaza Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga Manispaa ya Sumbawanga, Mei 30 mwaka huu au wiki ya kwanza ya Juni, 2020 fainali za FA zitafanyika huko huku mgeni maalumu akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/601db7901b4d937931568288e5e658ba.jpeg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi