loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mourinho: Timu bora imefungwa

JOSE Mourinho, amesema Southampton ndio ilikuwa timu bora kufuatia ushindi wa Tottenham wa mabao 3-2 katika mchezo wa marudiano wa raundi ya nne wa Kombe la FA juzi.

Vijana wa Mourinho walionekana kama wako nje ya mashindano hayo zikiwa zimebaki chini ya dakika 20 wakati mabao ya Watakatifu hayo yaliyofungwa na Shane Long na Danny Ings yalipobadili la Jack Stephens la kujifunza.

Lakini Lucas Moura alisawazisha kabla Heung-Min Son kuiahakikishia Spurs ushindi ambao umeiwezeha timu hiyo sasa kucheza dhidi ya Norwich mwezi ujao baada ya kufunga kwa penalti.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mourinho alisema: “Timu bora imefungwa. Timu bora uwanjani imefungwa. Ukiangalia kwa makini walicheza vizuri na walikuwa na wachezaji wazuri na timu iliyokamilika.”

“Tulikuwa katika matatizo makubwa, kujenga timu baada ya mchezo wetu dhidi ya Manchester City, ikiwa utasahau jambo kubwa kama hili, basi ujue timu bora ndio iliyopoteza mchezo.”

“Wao walikuwa wazuri sana kuliko sisi, walikuwa na kazi kuliko sisi na kiujumla walituzidi karibu kila kitu na walipata nafasi.”

Wakati huohuo, Dele Alli amesema Tottenham wanastahili kutwaa taji na kumaliza ukame wa miaka 12 wa kutokuwa na taji lolote. Spurs, katika mchezo wa juzi wa Kombe la FA ambao waliifunga Southampton 3-2 na kutinga hatua ya raundi ya tano, hawajashinda taji lolote tangu walipotwaa Kombe la Ligi mwaka 2008.

“Tunatakiwa kushinda kitu kwa ajili ya mashabiki. Tunastahili taji, ni muda mrefu tangu tulipotwaa kwa mara ya mwisho, tunatakiwa kupambana ili kushinda taji,” alisema.

Pamoja na kushindwa na Liverpool kwa kufungwa 2-0 Juni mwaka jana katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Tottenham ilimaliza ya pili katika Ligi Kuu ya England msimu wa mwaka 2016/17 na kucheza fainali ya Kombe la Ligi.

Baada ya siku chache Ozil kutojumuishwa kwenye orodha ya wachezaji ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi