loader
Christian Eriksen Afuata mataji Inter Milan

Christian Eriksen Afuata mataji Inter Milan

CHRISTIAN Eriksen anasema kuwa ameamua kujiunga na klabu ya Inter Milan kwa sababu ana nafasi kubwa ya kushinda mataji kuliko alivyokuwa Tottenham.

Eriksen alijiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia ya Serie A mwezi uliopita kwa ada ya uhamisho ya kiasi cha pauni milioni 16.9, ambacho kitamwezesha kuichezea timu hiyo kwa miaka minne na nusu.

Mkataba wa mchezaji huyo hapo Spurs ulikuwa unatarajia kumalizika katika kipindi kijacho cha majira ya joto. Sasa atakuwa katika klabu yenye maskani yake San Siro. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark alimaliza nafasi ya pili akiwa na Tottenham katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita na Kombe la Ligi mwaka 2015. Eriksen anasisitiza kuwa kuondoka kwake Spurs kunatokana na kiu yake ya kupata maji na anaamini kuwa Inter Milan itamwezeha kumaliza kiu yake hiyo.

“Kwa kweli kuna nafasi kubwa sana ya kushinda mataji hapa au kuna nafasi tele kuliko kule nilikotoka, ni kweli hapa kuna nafasi kubwa,” alisema Eriksen alipozungumza na Sky nchini Italia. “Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ilikuwa siku mbaya sana, kushindwa, ambako kamwe sipendi kuikumbuka …”

“Niko hapa kwa ajili ya kushinda na kuanza kitu fulani kipya. Kwa mara ya mwisho nilishinda kitu fulani nikiwa Ajax, hivyo ni miaka mingi sana imepita. Bado nakumbuka hisia zilizokuwepo wakati ule, hivyo nataka kushinda tena hapa.”

UHAMISHO WAKE

Katika dirisha la uhamisho la hivi karibuni kabisa, Eriksen alikuwa akishuhudiwa kuhusishwa na klabu kibao ikiwemo Real Madrid na Barcelona. Lakini anasema kuwa Inter Milan ndio walijitokeza mbele na ofa nono kuliko klabu zingine.

“Nilikuwa nahusishwa na klabu kibao katika misimu iliyopita. Wakati Inter walipokuja walikuwa wamekamilika na walionekana kuvutiwa zaidi,” alisema mchezaji huyo.

“Nilijiona mwenyewe nikicheza hapa, ilikuwa rahisi kusema ndio na bila shaka nimekuja hapa kujaribu na kushinda kitu fulani. “Nina furaha kubwa kukutana na Conte (kocha wa Inter Milan) hapa.

Niliambiwa awali kuwa ni mahali pagumu, lakini nilikuwa na vipindi vichache na katikati ya msimu ulikuwa mgumu ukilinganisha na Pochettino (aliyekuwa kocha wa Spurs). “Hadi sasa kuna kukimbia na mpira lakini Poch alikuwa sawa kama hapa. Kuna usawa lakini naona tofauti ya soka.

“Sipendi kukimbia. Napendelea kukimbia na mpira na kuwa na mpira wa kuchezea, lakini hilo litakuja tu. “Najua wakati wa kucheza dhidi ya Chelsea lilikuwa jambo gumu. Dhidi ya Conte, hasa, wanapocheza wachezaji watano nyuma na unajua mpira unapokwenda kwa beki wa pembeni wanaanza kutengeneza nafasi.”

MSIMAMO WA LIGI

Inter Milan katika msimamo wa Ligi Kuu ya Italia iko nyuma ya vinara Juventus, licha ya klabu hiyo yenye maskani yake Turin kushinda mataji nane ya ligi yaliyopita, Eriksen anaamini kuwa timu yake ina nafasi ya kuwa bingwa wa Italia.

Anasema: “Nafikiri kuna uwezekano. Tunatakiwa kucheza mchezo mmoja kwa wakati. Juventus imeshinda taji la Ligi Kuu kwa miaka mingi sasa. “Tunatakiwa kuwa na muendelezo na kuwakaribiakwa jinsiiwezekanavyona mwishoni tutaona tutaishia wapi.”

KOCHA MOURINHO

Kocha wa sasa wa Tottenham, Jose Mourinho anabainisha kuwa ilikuwa vigumu kumzuia Eriksen kuondoka, kwani tayari alikuwa ameshaamua kutoendelea kubaki Tottenham. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye amebakisha chini ya miezi sita katika mkataba wake na Spurs, alitua rasmi Inter Milan wiki iliyopita.

Baada ya kuondoka kwa mkali huyo, Spurs ilijibu kwa kumpa mkataba wa kudumu Giovani Lo Celso ambaye alikuwa akiichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Real Betis, huku wakimchukua Steven Bergwijn kwa ada ya pauni milioni 25 kutoka PSV Eindhoven.

KOCHA AMPONGEZA

Mourinho alipongeza tabia ya Eriksen katika miezi yake ya mwisho ya kuichezea Spurts. Aliniambia: “Siku nilipowasili hapa (Spurs) aliniambia kuwa sitaongeza mkataba tena. “Christian aliniambia tayari uamuzi ulishafanywa na hakuna njia nyigngine yoyote.

Kuanzia wakati huo nilikuwa najaribu kujenga timu bila ya kuwepo yeye. Hiyo ndio sababu kwanini sikuwa namchezesha mara nyingi.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/364a68b0135b3e768b603360fa3367bd.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: MILAN, Italia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi