loader
Picha

Serikali yajipanga kukabili uwezekano uvamizi wa nzige

BAADA ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Rwanda (RMA) kutangaza uwezekano wa nchi hiyo kuvamiwa na nzige, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO), imeanza kufuatilia kwa karibu taarifa za mienendo ya wadudu hao.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya nchi jirani na Uganda kuvamiwa na wadudu hao waharibifu wa mazao, ikiwa ni mwezi mmoja tangu walipovamia nchini Kenya. Wiki iliyopita, RMA ilitangaza wadudu hao wanatarajiwa kuvamia nchini humo kati ya siku 10 hadi 14 zijazo kutegemeana na hali ya hewa.

Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hali ya Hewa, Matthieu Mugunga, alisema mwenendo wa wadudu hao unafuatiliwa muda wote, huku wakitarajia katika siku 10 zijazo kuwa wamefika nchini humo.

“Kwa kuwa bado nchi ni kavu kama ilivyo Uganda, nzige wanaweza kufika Rwanda katika siku 10 mpaka wiki mbili zijazo, lakini kama mvua zitanyesha na kuwa na unyevunyevu hawataweza kusambaa kwa haraka,” alisema.

Mugunga alieleza uwezekano wa wadudu hao kufika nchini humo katika muda huo uko chini kwa asilimia 10 mpaka 20. Wakati huo huo, Wizara ya Kilimo imeeleza kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, kwa kushirikiana na taasisi nyingine inaendelea kufuatilia mwenendo wa wadudu hao.

Wizara hiyo imewashauri wakulima kutembelea mashamba yao kila siku na kutoa taarifa kama wataona wadudu wasio wa kawaida ili kupata msaada kwa kupiga simu ya wizara 4127 au kuwataarifu washauri wa kilimo walio karibu.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi