loader
Picha

Simba, Yanga hesabu kali leo

TIMU za Simba na Yanga leo zitakuwa na kibarua kigumu cha kutafuta ushindi wa pointi tatu muhimu ili kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania taji la Ligi Ligi Kuu Tanzania Bara.

Bingwa mtetezi Simba, wenyewe watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakicheza dhidi ya Kagera Sugar, wakati watani zao Yanga baada ya kujeruhiwa kwa kulazikishwa sare dhidi ya Tanzania Prisons watakuwa mjini Moshi kwenye Uwanja wa Ushiriki kucheza dhidi ya Polisi Tanzania.

Katika michezo hiyo kila timu inahitaji matokeo mazuri ambapo Simba wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 56 wanahitaji ushindi ili kuendelea kutanua kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, wakati Yanga wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi 39 wataingia kwa lengo la kusaka ushindi utakaowasaidia kupunguza utofauti wa pointi na kinara wa ligi.

Mechi ya Simba na Kagera wanakutana kwenye mchezo huo kila mmoja wao akiwa na morali ya juu baada ya kushinda michezo yao iliyopita. Licha ya Simba kuwa mwenyeji, lakini mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na historia yao ingawa walipokutana mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba walishinda kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amepania kulipa kisasi kwa Simba kwenye mchezo huo, ambao wanatarajia utakuwa kama fainali kwao.

“Mchezo utakuwa kama fainali kwetu, kwani tunacheza na timu inayopigia mahesabu ubingwa wa ligi, sisi tunakuja tukiwa tumejipanga kwa kuwaheshimu wapinzani wetu na hasa tukikumbuka kichapo cha nyumbani cha mabao 3-0, “alisema Maxime.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu lakini kikosi chake kilichowasili mapema juzi kipo sawa na wamepata maandalizi mazuri pamoja na kuwapa mbinu zitakazo wafanya kupata ushidi dhidi ya Simba.

Naye Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck baada ya kupata ushindi mchezo uliopita alisema matokeo mazuri waliyopata kwenye michezo miwili ya ugenini, wachezaji wake wapo sawa kisaikolojia hivyo utakuwa mchezo mgumu ingawa wanapigia mahesabu ushindi.

Kwa upande wa Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wa 21 wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare michezo miwili iliyopita dhidi ya timu za Mbeya, leo wanakutana na Polisi Tanzania wakipania kutoka na pointi tatu ili kurejesha matumaini kwa wapenzi wao.

Kuelekea kwenye mchezo huo kocha wa Yanga, Luc Eymael alisema wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo moja la kutafuta matokeo mazuri na kufuta wimbi la kupata sare walizopata michezo miwili ya ligi hiyo.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu, kwani walipokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wawili hao walitoka sare ya kufungana mabao 3-3 mechi iliyofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Michezo mingine sita ya ligi hiyo inatarajiwa kuendelea, ambapo Mbao watakuwa wanakabiliana na Singida United, wakati Coastal Union na Ruvu Shooting, Mbeya City na Lipuli FC, JKT Tanzania na Biashara wakati Namungo dhidi ya KMC.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

2 Comments

 • avatar
  Malima bilinje
  18/02/2020

  Naitakia ximba uxhnd leo

 • avatar
  Maulid
  18/02/2020

  Naitakia ushindi simba leo pia nakanusha kauli ya haluna niyonzima akidai kua kila tim atakayo kwenda lazima ichukue kombf la vpl haya ackukue sasa kama kwel anabahat

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi