loader
Picha

Twiga Stars kuikabili Morocco leo

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar Stars’ Bakari Shime amesema kushambulia kwa kasi ni moja ya mbinu anayotegemea kuitumia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Morocco unaotarajia kufanyika kwenye Uwanja wa Kram nchini Tunisia.

Shime ametoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi kwenye mechi iliyopita kwa mabao 3-2 dhidi ya Algeria ukiwa ni muendelezo mzuri wa matokeo kufuatia kuanza vyema michuano hiyo kwa kuwafunga Mauritius kwa mabao 7-0 kwenye muendelezo wa mashindano ya Kanda ya Kaskazini (UNAF).

Alisema anajua wapinzani wao hao wana maumbile makubwa na vikosi vyao vinaundwa na wachezaji warefu ukilinganisha na wachezaji wake, hivyo anaamini kupitia mbinu hiyo ana uwezo wa kutibua mipango na kupata ushindi.

“Nimegundua wachezaji wangu wamezidiwa kwenye maumbile makubwa, hata urefu na tunaenda kukutana na Morocco najua ni wazuri, lakini mbinu pekee ya kuendeleza ushindi ni kuwashambulia kwa kasi muda wote, ” alisema Shime.

Shime licha ya kuwapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri waliyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Algeria anadai nyota wake walipata shida, hasa kwa kitendo cha kuruhusu kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.

Baada ya mchezo huo wa leo dhidi ya Morocco kikosi cha Twiga Stars ambao ni wageni waalikwa kwenye michuano hiyo, watabaki na mchezo mmoja dhidi ya wenyeji Tunisia, ambao utachezwa keshokutwa.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi