loader
Picha

Kivumbi usiku wa Ulaya leo

KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya 16 bora kinatarajia kutimka leo na kesho kwenye viwanja tofauti wakati timu nane zitapochuana.

Kipute kikali kinatarajia kuonekana pale Atletico Madrid itakapochuana na vinara wa Ligi Kuu ya England, Liverpool katika mchezo utakaofanyika Hispania. Timu hizo zinasaka nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo katika mbio za kuwania ufalme wa Ulaya msimu huu.

Kikosi cha kocha Diego Simeone kinataka kuonesha umwamba dhidi ya kile cha Klopp, ambacho mbali na kuongoza kwa mbali katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, pia ndio mabingwa watetezi wa Lgi ya Mabingwa wa Ulaya.

Hatahivyo, Atletico Madrid wako pointi 12 nyuma ya vinara Real Madrid katika msimamo wa La Liga na wiki iliyopita walikaa katika nafasi ya sita. Katika mchezo mwingine leo, Borussia Dortmund itacheza dhidi ya PSG wakati Atalanta itacheza dhidi ya Valencia katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa San Siro.

Nayo Tottenham Hotspur itakuwa mwenyeji wa RB Leipzing katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya utakaofanyika kesho.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi