loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uganda yawatumia fedha wanafunzi waliopo China

SERIKALI ya Uganda imesema itatuma Dola za Marekani milioni 60 ili kuwasaidia wanafunzi wake waliokwama katika mji wa Wuhan, nchini China, uliowekwa chini ya karantini kutokana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa hatari wa corona.

Raia wa Uganda wameanzisha kampeni ya ‘Okoa Waganda Wuhan’, baada ya wanafunzi wa nchi hiyo waliopo katika mji huo kueleza kukosa chakula na vifaa kama maski za usoni za kudhibiti virusi hivyo.

Inakadiriwa kuwa, kuna takribani raia 105 wa Uganda katika mji huo ambao ndio chanzo cha mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona. Juzi, Waziri wa Afya wa Uganda aliliambia Bunge la nchi hiyo kuwa, takriban Dola za Marekani 60,000 zimetumwa kusaidia wanafunzi wa nchi hiyo waliopo katika mji huo wa China, ingawa haijulikani kila mwanafunzi anapata shilingi ngapi.

Serikali ya Uganda imeeleza kwamba, kuwarudisha nyumbani raia wake kutoka Wuhan kunaweza kusababisha maambukizi hayo kufika Uganda na kwamba miundombinu ya taifa hilo haiwezi kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo endapo utatokea.

Katika mataifa mengi, vipimo vya virusi vya ugonjwa huo vimewekwa katika viwanja vya ndege ili kudhibiti ugonjwa huo kuingia kupitia abiria wanaotoka mataifa mengine. Karibu watu 1,700 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali duniani hasa China ambako ndiko chimbuko lake, huku wengine zaidi ya 70,000 wakithibitishwa kuwa na virusi hivyo wengi wao wakiwa China.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba ugonjwa wa corona ni janga la kimataifa na linahofia kwamba nchi maskini huenda zikashindwa kukabiliana na mlipuko huo.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi