loader
Picha

Dk Mashinji atoa sababu kuhama Chadema

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Vincent Mashinji ametangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dk Mashinji aliingia katika chumba cha mikutano Lumumba akiwa amevaa fulana yenye nembo ya Chadema na baada ya kupokelewa rasmi, alienda kubadili na kuvaa ya CCM.

Mashinji ambaye amepokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika Ofisi Ndogo za Lumumba, Dar es Salaam amesema ameamua kuhamia CCM kutokana na kukosekana kwa maridhiano ndani cha Chadema.

“Nimekaa nikatafakari jinsi ambavyo ndani ya chama hiki tunalumbana asubuhi hadi jioni, jambo ambalo linatuchelewesha,” huku akiongeza, “Nimeona kuwa CCM kuna utayari wa kuendeleza Watanzania wakati huku nilikotoka utayari huu siuoni.”

Ameeleza pia kuwa nia yake kubwa kuhamia CCM ni kuwa miongoni mwa Watanzania wanaotumia fursa ya kuchangia maendeleo ya nchi.

MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi