loader
Picha

Serikali yaeleza inavyothamini wachimbaji Tanzanite

SERIKALI imesema inawathamani wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite katika migodi iliyopo Mirerani wilayani Simanjiro kwani wameinyanyua sekta hiyo kimapato pindi wachimbaji wakubwa waliposusa kuchimba.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati akikabidhiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi jengo la kituo cha pamoja cha biashara cha madini ya tanzanite lililojengwa Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (Suma JKT) kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.3.

Biteko alisema baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini waliposusia kuchimba madini, wachimbaji wadogo waliendelea na shughuli zao na kuongeza maradufu mapato ya madini nchini.

Alisema Kampuni ya TanzaniteOne kabla ya kufunga mgodi wao walikuwa wanalipa Sh bilioni 1.1 na wachimbaji wadogo walikuwa wakilipa zaidi ya Sh milioni 164, lakini sasa wachimbaji wadogo wakawapita wachimbaji wakubwa na kufikia mapato ya zaidi ya Sh bilioni 2.7.

Aliwaomba wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite kuendelea kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ili serikali iendelee kuingiza mapato na kufanya maendeleo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Mwinyi aliwashukuru viongozi wa Wizara ya Madini kwa kuwapa heshima ya kujenga miradi mbalimbali ya madini.

“Pamoja na hayo nawapongeza maofisa wa jeshi na askari wengine ambao wamefanikisha ujenzi wa kituo hiki cha pamoja cha kisasa ambacho tunawakabidhi leo Wizara ya Madini,” alisema Dk Mwinyi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Chelestino Mofuga amempongeza Waziri Biteko kwa kusimamia sekta ya madini ambayo hivi sasa inatambulika kama sekta rasmi kwa kuingiza mapato ya nchi.

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, James Ole Millya amesema bado ana imani kubwa na Waziri Biteko kutokana na kusimamia rasilimali ya madini ambayo inawanufaisha wachimbaji wa eneo hilo.

Ole Millya alieleza kuwa tangu Biteko alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Spika mwaka 2017 hadi sasa hajawageuka wachimbaji wadogo na amekuwa nao bega kwa bega.

MKURUGENZI wa Wakala wa Misitu Tanzania, TFS, Santos Salayo ameonya ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Simanjiro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi