loader
Dstv Habarileo  Mobile
Utafiti wabainisha hatari inayowakabili watoto wanaochelewa kulala

Utafiti wabainisha hatari inayowakabili watoto wanaochelewa kulala

UTAFITI mpya unaonyesha kuwa watoto wanaochelewa kulala usiku wako kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo la uzito uliopita kiasi.

Hata hivyo, mmoja ya watafiti na mwandishi wa utafiti huo ambaye ni Profesa wa magonjwa ya watoto kutoka Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden, Claude Marcus amesema wazazi sio lazima waanze kuwalaza watoto wao mapema bali watengeneze ratiba endelevu ya muda kulala.

Kwa mujibu wake, hatari hii ni kwa watoto walio chini ya miaka sita.

Utafiti huo mpya ambao umechapishwa kwenye jarida la Pediatrics ulijikita kwenye tatizo la uzito uliopitiliza ambao ulihusisha watoto 107 nchini humo, 64 kati yao wakiwekwa kwenye kundi la wenye tatizo hilo la kiafya.

Waligundua kuwa watoto waliokuwa na tatizo hilo, moja ya tabia waliokuwa nayo ni ya kwenda kulala zaidi ya saa tatu usiku.

Profesa Marcus amesisitiza kuwa hiyo siyo sababu pekee ya kusababisha shida hiyo kiafya lakini, bali ni jambo linalowaweka watoto kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo hilo.

Sababu nyingine ni za kibailojia pamoja na mitindo ya maisha ikiwa ni pamoja na aina za vyakula watoto wanavyolishwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a719305c707ee6c6845864a38e577512.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi